HATUA YA 146: Wakati Mwingine Unahitaji Kitu Hiki ili Usonge mbele.

jacobmushi
2 Min Read
Kuna nyakati tunapitia magumu mengi sana kwenye Maisha hata unatamani kuacha kabisa kile unachokifanya. Kama huna maono imara unaweza kujikuta unarudi nyuma mara moja.
Ili uweze kupiga hatua yeyote kubwa lazima KUJIAMINI kuhusike kwa kiasi kikubwa sana. Kama hujiamini hata kama una bidhaa nzuri kiasi gani wakati mwingine utashindwa kuielezea mbele ya mteja.
Kama hujiamini kuna wakati utakutana na fursa nzuri na ukakosa ujasiri wa kujieleza unachokifanya. Kujiamini kunakuja pale unapokifahamu vizuri kile unachokifanya na kuamini kwamba unaweza. Kama ukianza kujikataa mwenyewe huwezi kuwaambia watu wakakukubali.
Kuna wakati watu wanaweza kuikosoa kazi yako au bidhaa yako kiasi kwamba ukaanza kukosa nguvu ya kuielezea mbele za watu. Hili lisikupe shida anza wewe mwenyewe kuwa mteja wako wa kwanza, anza kuona vitu vizuri vilivyopo ndani ya ile bidhaa unayoiza. Vitu hivyo ndio vikupe wewe ujasiri na kujiamini pale unapoelezea mbele ya mteja wako.
Mojawapo ya vitu ambavyo vinasababisha watu wengi washindwe kujiamini ni pale mtu anapotazama Zaidi madhaifu yake kuliko yale mazuri aliyonayo. Kila mtu ana madhaifu kama ukitumia nguvu nyingi kuangalia madhaifu ya mtu utayaona tu. Hivyo wewe ni kuona mambo mazuri uliyonayo na uyaonyeshe Zaidi yafunike madhaifu yako.
Kingine ni historia mbaya ya nyuma, kama mtu alishapitia mambo mbalimbali kama kushindwa kwenye masomo au biashara, kukataliwa na mengineyo mtu huyu anaweza kukosa kujiamini kabisa. Unatakiwa uanze kujijengea tabia ya kujiamini wewe mwenyewe. Hakuna mtu atakuamini kabla hujaanza kujiamini wewe mwenyewe.
Kitu cha msingi unachotakiwa kuwa nacho makini ni kutokujiamini kupitiliza hadi ukashindwa kuangalia unapokosea na kurekebisha. Lazima uweze kujifanyia tathimini uone sehemu za kurekebisha na kuongeza viwango.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Chukua Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Usiishie Njiani Academy https://jacobmushi.com/whatsapp/

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading