Yapo mambo ya muhimu unayopaswa kuyajua na kuyafanyia kazi kila siku ili usiishie njiani. Fanyia kazi mambo haya na Maisha yako hayatakuwa kama yalivyo kuwa.

Tambua Kusudi lako.

Kitu cha kwanza wewe kama mwanadamu unapaswa kutambua ni kwamba ulizaliwa kwa kusudi maalum. Kwa vile hakuna aliezaliwa na mwongozo kwamba yeye amekuja huku duniani kufanya nini, ni jukumu la kila mmoja kutafuta kwanini yeye yupo duniani.

Hakikisha unatambua kusudi lako hapa duniani huu ndio msingi wa kwanza wa Maisha yenye mafanikio. Kufahamu Zaidi juu ya Kusudi lako soma Kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo. Ndani ya kitabu nimeelezea kwa upana njia gani za kutambua kusudi lako, vitu gani vinaonyesha unachokifanya sio kusudi lako.

Kuwa na Maono Makubwa.

Ukishatambua kusudi lako tengeneza picha kubwa ya ukamilisho wa kusudi lako. Jione ukiwa umefikia mafanikio kwenye hilo kusudi lako. Ukishakuwa na picha kubwa ambayo ni maono hapa unakuwa kama umeshapata ramani ya kule unakotaka kuelekea. Huwezi kuyumbishwa na watu. Utajua ni vitu gani sahihi vya kufanya.

Utatambua ni gharama kiasi gani unapaswa kulipa ili ufikie maono hayo. Ni muhimu sana kila mmoja kuwa na maono na kuyafanyia kazi kila siku ili tuweze kuacha alama kwenye dunia hii.

Zungukwa na Waliofanikiwa Zaidi Yako.

Hakuna namna ambayo unaweza kujifunza kama utakaa na watu ambao mnafanana karibia kila kitu. Kama wewe una udhaifu Fulani tafuta watu au mtu ambaye yuko vizuri sehemu ambayo ni udhaifu wako. Kaa na watu ambao wameshafanya mambo makubwa hii itakupa hamasa ya kufanya makubwa Zaidi.

Ukikaa na watu ambao mnafanana kila kitu hata mazungumzo yenu yatakuwa ni yale yale. Hakuna hata mmoja anaeweza kuja na kitu kipya cha kuzungumza. Hakuna ambaye ataleta mawazo mapya maana wote mnafanana.

Jifunze kila Siku.

Jifunze kila siku kwa kupitia vitabu, audios, videos, soma Makala. Jifunze kwa kupitia hadithi za wengine. Angalia wengine wanakosea wapi ili wewe ufanye vizuri Zaidi.

Jitengenezee ratiba yako ya kujifunza kila siku. Jua ni vitabu gani vya muhimu Zaidi kwenye kile unachokifanya na uwe unasoma mara kwa mara. Matatizo mengine unapitia majibu yako yapo kwenye vitabu.

Jiunge na Group Letu 

Ukijiunga na group letu la WhatsApp utapata mafunzo, semina na ushauri wa kila siku ambao utakusaidia kwenye kile unachokifanya uweze kupiga hatua kila siku na ufikie mafanikio.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/coach

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading