Kamwe usikubali kuwa mtu ambaye anadanganya. Mtu mwongo atakula matunda ya kinywa chake, uongo ni mbegu na inazaa mazao yake. Matokeo ya uongo ni kushindwa kuaminika. Matokeo ya uongo ni kujishushia heshima, matokeo ya uongo yanaweza kuwa makubwa sana hasa kama una maono makubwa. Kuna mambo yako yatashindwa kwenda kwasababu ulidanganyaga kipindi cha nyuma.
USIKUBALI KUWA MWONGO.

Wewe ni Binti vile unavyojiweka mbele ya wanaume ndivyo wanavyokuchukulia hata kama sio tabia yako hiyo. Vile unavyojirahisisha ndio wanaona huyu ni wa kutumia siku moja tu unapita hivi sasa wewe utabaki unalalamika kusema wanaume hawafai. Ukiwa mgumu ukakataa kujirahisisha hovyo watakuja wenye maana. Sio kila anaekutongoza anakutaka wengine wanataka wajue wewe ni mtu wa namna gani unajirahisisha hovyo. Unaingia kwenye mtego kwa kununuliwa msosi tu basi wanaondoka na picha hiyo kichwani mwao.
BINTI USIKUBALI KUJIRAHISISHA, THAMANI YAKO INASHUKA.

Usiwe mtu wa maneno mengi, kwani kadiri unavyoongea ndivyo maneno yasiyofaa unakaribia kuyatoa sasa hatuna kipimo ukishaongea maneno kiasi gani ndio yanatosha. Wewe jiwekee kipimo chako mwenyewe hapa  ndio mpaka wangu siuvuki. Maneno yako ndio wewe ulivyo. Kile unachopenda kuzungumza sana ndio utakuwa hivyo. Ukipenda mizaha na huna mpango wa kuwa mchekeshaji unatarajia nini? Ukiongea sana kaa chini utafakari sana utakuta kuna sehemu uliongea kwa makossa punguza maneno, maneno ni mbegu.
NENO NI MBEGU, UNAPANDA NINI KWA WATU?
Usiwe mtu wa kujikweza unajua kwamba vyote ulivyonavyo umetafuta kwa bidii sawa lakini ukiashaanza tabia ya kujiona umeshafika na kudharau walioko chini yako utaanguka. Kilichokufikisha hapo ulipo sio wewe mwenyewe ni michango ya watu wengi. Ni watu waliomini kile unachokifanya, iwe ni biashara au kipaji chako. Kuna watu waliamini bidhaa unazotoa wakaamua kuja kununua kwako. Kuna watu waliamini kipaji chako wakaamua kuwa mashabiki zako. Usijikweze na kujiona umejifikisha hapo ulipo peke yako utadondoka haraka sana.
KUNA WATU WAMEKUNYANYUA UKIANZA KUWA KURUKARUKA JUU YAO WATAKUACHIA UTAANGUKA.
Karibu sana rafiki Yangu.
#USIISHIE_NJIANI.
Jina: Jacob Mushi
Kazi: Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.
Simu: 0654726668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading