HATUA YA 187: Bado Nafasi Ipo.

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read
Kama Umeamka tena leo basi bado nafasi ipo. Bado nafasi ya kubadilisha pale ulipokosea tena. Usiogope wala kukata tamaa kwa lolote lile kama bado unapumua ni ujumbe kwamba unayo nafasi ya kufanya mabadiliko kwenye Maisha yako.

Haijalishi umepitia mangapi ya kukuvunja moyo wako na kukurudisha nyuma kama bado hujafa yaani bado upo hai. Huo ni ujumbe ya kwamba nafasi ya kufanya mabadiliko ipo, nafasi ya kuendelea na mapambano ipo.
Hata kama umeanguka mara ngapi bado unayo nafasi ya kuendelea tena na pambano tena. Uhai wako ni ujumbe kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwamba uendelee mbele. Rekebisha pale ulipokosea ili usiendelee kuanguka tena.
Bado nafasi ipo ya kutengeneza Maisha unayoyataka. Bado nafasi ipo ya kufanya kile unachotamani kukifanya.
CHUKUA HATUA.
Japokuwa nafasi ipo lazima uamue kuchukua hatua. Anza sasa kuinuka hapo ulipoangukia. Anza sasa  kufanya chochote unachoweza ili kuifanya ndoto yako iwe kweli. Hakuna kingine ndugu yangu Zaidi ya kuanza kufanya. Hakuna kingine Zaidi ya kufanya vitendo.
Machozi hayatasaidia, lawama hazitasaidia, majuto hayatasaidia, sababu hazitakufanya usonge mbele. Kuchukua hatua pekee yake ndio kutakufanya wewe usogee.
Haijalishi ni kwa kiasi gani umepata hasara au umeumizwa kukaa chini na kulia hakutabadilisha chochote. Mabadiliko yatakuja pale tu utakapoanza kufanya vitu.
#USIISHIE NJIANI
Usiache kusoma Kitabu cha Siri 7 za kuwa hai leo wasiliana nami kwa 0654726668.
Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali na Mhamasishaji.
Simu: 0654726668
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading