Tatizo la wengi na linasosababisha tunapotea katika vitu visivyoeleweka ni kutokuuliza maswali. Wewe kama mwanadamu tofauti yako na Wanyama wengine ni uwezo wako wa kufikiri. Sasa kama mtu atakuja akasema kitu na wewe ukakifuata tu bila ya kujiuliza na kitu hicho hukijui ni kipya kwako inakuwa rahisi sana kupotezwa.

Mfano umekwenda hospitali kumwona Daktari usikubali kwa vyovyote vile ulazimishwe kufanya maamuzi kwasababu tu aliesema ni daktari kama jambo hujaelewa uliza swali kwa utaratibu mzuri. Unaumwa kichwa daktarin akasema vua nguo panda kitandani. Lazima ujiulize kichwa na kuvua nguo ni wapi na wapi? Uliza swali usivue nguo tu kwasababu amesema Daktari huo ni mwili wako sio chombo cha majaribio. Kwanini nivue nguo wakati naumwa kichwa?

Watu wengi wamekuwa wanatapeliwa kwasababu hawaulizi maswali. Ili uweze kuuliza maswali vizuri usikubali kuendeshwa na hisia. Hakikisha akili yako inafanya kazi sawasawa kabla hujafanya maamuzi.

Kwenye Biblia kuna andiko linasema “Watu wangu Wanaangamia kwa kukosa maarifa” kwa kukosa maarifa ndani ya kichwa chako ndipo unaweza kujikuta umebebwa na watu waliofikiri Zaidi yako.

Ukishindwa kuuliza maswali basi utajikuta unapelekwa na kila kinachokuja kila unachoambiwa. Maisha yako yatakosa msimamo unaoleweka. Jifunze kuuliza maswali kwani ndio chanzo cha kukua kiufahamu. Haijalishi utaonekana wewe ni mjinga au hufahamu lakini baada ya kuuliza huwezi kubakia vile ulivyokuwa.

Jifunze kuuliza maswali vizuri ndio utapata majibu mazuri. Utajibiwa kutokana na ulivyouliza, ukikosea kuuliza maswali utapokea majibu kimakosa. Uliza maswali ndio utaweza kuwafahamu watu na kujitengenezea fursa nyingine nyingi Zaidi.

Jiulize wewe mwenyewe maswali kila siku kwenye kile unachokifanya ili uweze kujielewa ulipo, unapoelekea. Jiulize maswali kabla hujafanya maamuzi yeyote ambayo yanagusa Maisha yako. kwa kujiuliza maswali ndio unapata usahihi wa kile unachotaka kufanya.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading