HATUA YA 225: Unautumiaje Muda wa Ziada?

jacobmushi
By jacobmushi
3 Min Read
Mojawapo ya sababu wengi wanaitumia juu ya kwanini hawana kitu kingine wanafanya ni kukosa muda. Lakini ukija kumuuliza maswali Zaidi unakuja kugundua huyu mtu ana muda mwingi wa kutosha ambao angeutumia angefanya mambo mengi sana.
Kama kweli wewe umeamua kubadilisha Maisha yako kuanzia sasa achana na kuangalia Tv, Acha kupoteza muda kufuatilia mambo ambayo unajua kabisa hayakuletei pesa wala faida yeyote baada ya kuyafahamu. Muda huo utumie kufanya yale unayotaka kuona yanatokea kwenye Maisha yako.
Badala ya kutumia masaa mawili unatazama Tv tumia muda huo kujisomea kitabu. Muda ambao unakuwa kwenye gari  ukisubiri foleni badala ya kupiga story tumia muda huo kuongeza kitu kwenye akili yako. tenga muda ambao utautumia kukutana na watu wapya ambao mnaweza kuzungumza biashara au mambo yenye manufaa kwenye Maisha yenu.
Usikubali kupoteza muda wako hovyo halafu unasema huna muda kabisa, uko bize, na sababu nyingine nyingi wakati Maisha ni yako mwenyewe. Hizo sababu hazibadilishi hali mbaya uliyonayo.
Kama wengine wanaamka kwa kuchelewa na wewe unajua kabisa huna muda wa kutosha amka mapema kuliko wengine. Ukiweza kuamka masaa mawili mapema Zaidi ya ulivyokuwa umezoea utaweza kufanya mambo mengi ya maana sana kwa ajili ya Maisha yako.
Huu muda unaoukoa unaweza kujiingiza kwenye biashara ambazo hazikulazimishi uzifanye muda Fulani pekee. Unaweza kutumia muda huo kuandika, au kuuza bidhaa zako kwenye mtandao. Unaweza kuutumia muda huo kuwapelekea wateja wako bidhaa. Unaweza kuutumia muda huo kuwashirikisha watu biashara yako, kama unafanya biashara ya mtandao (NETWORK MARKETING).
Huu muda wa ziada kama wewe ni mwajiriwa na una ujuzi mwingine wa Ziada unaweza kuutumia kutengeneza kile ambacho unakifahamu na kwenda kukiuza kwa wateja wako kwa muda mwingine. Unaweza kuutumia muda huu kuuza kile ambacho umekitengeneza.
 Wakati mwingine inakubidi ujitoe Zaidi yaw engine. Kna nyakati itakupasa uamke wakati wengine wamelala ili uweze kufika kule unakotaka. Kama hakuna kitu cha tofauti unafanya Maisha yako hayawezi kubadilika yataendelea kuwa hivyo yalivyo siku zote.
Inakubidi ufanye mambo magumu yale unayoyaogopa maana hayo ndio yenye matokeo makubwa juu ya Maisha yako. amua sasa anza kuchukua hatua.
Jacob Mushi
#USIISHIE_NJIANI
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading