HATUA YA 23: Unataka kwenda Mbali au Unataka Kufika Haraka?

jacobmushi
2 Min Read
Kuna msemo mmoja unasema kwamba “Kama unataka kufika haraka nenda/tembea mwenyewe. Kama unataka kufika mbali usiende peke yako nenda pamoja na wengine.

 “If you want to go quickly, go alone. If you want to go far, go together.”

Ukienda peke yako Hutafika mbali, hutaenda mwendo mrefu utachoka. Kama safari yako ni ndefu usichague kwenda peke yako. Kama safari yako ya mafanikio ni fupi wewe unaweza kwenda mwenyewe utafika haraka tu bila tatizo.

Unahitaji watu ili kufika kule unapotaka kwenda haijalishi umefika wapi. Hii ni kwasababu unachokitafuta sio kwa ajili yako pekee. Hakuna mafanikio ya mtu ambayo hayagusi Maisha ya wengine.

Nionyeshe mtu mmoja ambaye amefanikiwa na hajafanyika namna moja kubadilisha Maisha ya wengine iwe kwa bidhaa au huduma yake.
Kama kuna mtu anataka mafanikio ya haraka ambayo hayagusi Maisha ya wengi siku zote safari yake inakuwa ni fupi.

Mtu mbinafsi pekee ndiye atataka afike kule aendako mwenyewe. Katika safari yako ya kutimiza ndoto zako unahitaji watu wengi sana ili ufike mbali. Watu hawa kila mmoja ana mchango wake wa tofauti kwenye ndoto yako.

Kumbuka: Sio kila mtu anafaa kwenda nae lazima ujue ni watu wa aina gani unawahitaji ili mfike kule uendako. Wengine wanaweza kuwa sababu ya wewe kupotea au kutokufika.

Pia kuna msemo unasema kama hujui unapokwenda usiwaambie watu wakufuate. Kama hujaelewe vyema uendako usiwaambie watu waende na wewe maana utawapoteza.
Karibu sana.
Your Partner in Success
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
jacobmushi.com.
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading