HATUA YA 234: Simama Upigane au Potea Kabisa.

jacobmushi
2 Min Read

Upoanguka wakati wa changamoto unakuwa na maamuzi ya aina mbili. Moja ni kusimama na kuendelea kupigania ushindi au kupotea kabisa. Unapoamua kupotea unakuwa umekubali ugumu wa kila namna uliopo hapa duniani. Unakuwa umekubali kuendelea kuwa maskini, kuishi maisha ya kawaida kama wengine.

Unapochagua kusimama na kuendelea na pambano unakuwa umeamua kupigania kile ambacho umesema unakitaka. Kuna tofauti ya kujificha na kukata tamaa, Biblia inasema kwenye kitabu cha methali 27: 12 Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia. 

Hivyo ni muhimu sana kutumia busara ambayo iko ndani yako kujua kama mabaya yanayokuja ni ya kupambana au ni ya kujificha ili yapite.

Unapokuwa katika pambana ukianguka unapaswa kusimama na kuendelea na pambana.

Zitazame faida utakazopata baada ya kumaliza pambano na sio maumivu unayosikia wakati huu unapopambana. Watu wengi wanakata tamaa kwasababu wanasikiliza Zaidi maumivu wanayopata kuliko yale maisha watakayokuja kuishi baada ya pambano.

Mpiganaji anapokuwa ulingoni haangalii Zaidi ngumi anazopigwa fikra zake zinakuwa Zaidi baada ya ushindi. Ukiweka fikra zako kwenye maumivu utakata tamaa. Weka fikra zako kwenye ushindi hasa pale unapokuwa umeanguka chini.

Unapojitazama ukiwa juu, ukiwa umebeba taji, ukiwa umeshapata kila ulichokuwa unakitaka, nguvu zitarudi upya na utaweza kuendelea na pambano.

Usikubali kuyasikilizia maumivu kuliko unavyoona ushindi.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading