HATUA YA 238: Kwanini Usifanye Maamuzi Hisia Zikiwa Juu?

Kuna aina nyingi za hisia kama hisia za hasira, furaha, hamasa, chuki, na nyinginezo unazozijua. Hisia zote hizi unaweza kuzigawa katika makundi mawili ili uelewe vizuri Zaidi, yaani Hisia Hasi na Hisia Chanya.  Hisia zozote zile ziwe za hasi au chanya zinaweza kuwa na madhara kwetu kama zitatufanya tuchukue hatua bila ya kufikiri.

Kama utajikuta maamuzi mengi unayochukua ni ukiwa na furaha sana unaweza kuja baadae kugundua ulipofanya ulikosea. Mfano umekuwa sehemu mkahamasishwa ukafurahi sana ukajikuta unatoa ahadi kubwa kuliko uwezo wako. Baadae akili zako zinaporudi sawa unakuja kugundua kwamba uliahidi kitu kikubwa sana kuliko uwezo wako.

Wataalamu wanasema hisia zinapokuwa juu uwezo wako wa kufikiria unakuwa chini. Hii ndio maana mtu anapokuwa kwenye hisia labda za kimapenzi anaweza kumuahidi mpenzi wake chochote, wengine huahidi watatoa dunia, na vingine vingi wasivyoviweza. Lakini ukija kwenye uhalisia unakuta yale aliyokuwa anaongea ni maneno yasiyowezekana.

Vilevile unapokuwa na hasira kali sana juu ya chochote akili zako zinakuwa chini yaani kuna kiwango cha ukichaa tunaweza kusema kinakuwa juu yako. Ona mtu mwenye hasira kali anaweza kuvunja vyombo  vya thamani, anaweza kupasua simu, anaweza hata kuchoma nyumba. Baada ya matukio haya kuisha yaani akili yake ikirudi sawa anakuja kugundua alikosea sana. Anaanza kujutia matendo yake aliyofanya.

Katika hisia zote hisia za kuwa nazo makini Zaidi ni hisia za hasira kwasababu ukiwa na hisia hizi maamuzi unayofanya yanakuwa kama ya mtu mwenye upungufu wa akili. Unaweza kuumiza watu, unaweza hata kuua kabisa.

Ushauri wangu ambao napenda kuutoa kwa mtu mwenye hasira kali sana unapoona hasira zinakuja juu nenda kafanye mazoezi makali yatakayokufanya utoke jasho na uheme. Au kunywa maji mengi sana wakati huo. Unaweza pia kwenda kuoga na maji ya baridi.

Kamwe usirihusu katika maisha yako ukawa unaogozwa na hisia kuliko akili. Maamuzi mengi utakayofanya yanaweza kuwa sio sahihi.

Kama ulishawahi kwenda sokoni au shoping ukajikuta umefanya manunuzi ya kitu ambacho hukuwa umepanga kununua baada ya kufika nyumbani ukaanza kujuta kununua kitu kile ujue pia ulifanya maamuzi kwa hisia. Hukushirikisha akili zako wakati unafanya maamuzi yale.

Usikubali kuhamasishwa kwanza ndipo ufanye maamuzi ambayo ynagusa maisha yako kwa kiasi kikubwa kwasababu pia hamasa ni aina ya hisia chanya. Ni vyema ukapata hisia za kutoka ndani yako kuliko hisia za nje yaani kutoka kwa watu wengine. Hamasa inayodumu Zaidi hata ukiwa peke yako ni hisia inayotoka ndani yako.

Unapokuwa na hisia kali penda kujipa muda kwanza hadi hisia zishuke ndipo ufanya maamuzi. Unaweza kutapeliwa kwa kuweka hisia juu, unaweza kuibiwa au kufanywa chochote kibaya kwasababu hukuweka akili yako sawa wakati unafanya maamuzi.

Hua napenda kuwaambia watu unapofanya maamuzi yeyote yanayohusu maisha yako tazama miaka 2-5 mbele angalia matokeo ya maamuzi yako ndipo ufanye maamuzi.

Ndio maana unapaswa KUFIKIRI, KUFIKIRI, KUFIKIRI TENA.

Kuwa Mwanachama Kamili wa Usiishie Njiani Bonyeza hapa.. www.jacobmushi.com/jiandikishe

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. www.jacobmushi.com/patavitabu

Jipatie Blog Bora hapa.. www.jacobmushi.com/jipatieblog

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

jacobmushi
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading