HATUA YA 239: UKipewa Nafasi Ya Kurudi Nyuma Utarekebisha Wapi?

jacobmushi
3 Min Read

Swali moja ambalo napenda kuwauliza watu ambao wako mbele Zaidi yangu kwenye mafanikio katika Nyanja zote, kiafya, kiroho, kimahusiano na pia kifedha au kwenye biashara ni “ Endapo ikatokea Umerudi nyuma kabisa ukatakiwa uanze upya kile unachokifanya sasa hivi, ni vitu gani hutavifanya kabisa ma ni vitu gani utawekea mkazo Zaidi kuliko vingine?”

Swali hili ni la ufahamu kwa mtu ambaye ameshasafiri na kufikia viwango Fulani anapaswa kujua ni mambo gani akiambiwa aanze tena safari yake hatayarudia kabisa nay epi hasa atawekea mkazo Zaidi. Kama umefika mahali na unashindwa kujibu hilo swali basi inawezekana hapo ulipofika hujui umefikaje.

Kama binadamu kila  mmoja ana safari yake kule anapoelekea. Unapopita katika pori ambako hakuna njia kabisa unaweza kukosea sana na hata kupotea kule unapoelekea. Unachopaswa kufanya ni kuendelea kuitafuta njia unapoipata njia unaanza kuwa na mwelekeo unaoeleweka. Na akama itatokea ukarudi tena kule ulikopita huwezi kupotea tena kwasababu umeshajua njia sahihi ni ipi na wapi ukipita utapotea.

Ni vyema sana tukatumia nafasi ya kujifunza kwa wale ambao wametutangulia katika vile vitu ambavyo tunataka kufikia mafanikio makubwa. Kila mtu ana mtu wake ambaye anaweza kujifunza kwake kulingana na safari yake hapa duniani.

Una uwezo na nafasi ya kujifunza ili usirudie makossa ambayo walishayafanya waliokutangulia. Ukiona unafanya makossa ya walikutangulia inawezekana hujajifunza vizuri kwao.

Jiulize leo ukipata nafasi ya kurudi nyuma miaka mitano au kumi ni vitu gani hasa ungetaka kuvibadilisha kwenye maisha yako? Ni hatua gani usingezichukua ambazo ulizichukua na zikasababisha uwe kwenye hali uliyonayo sasa hivi?

Ukweli ni kwamba huwezi tena kurudi nyuma bali unaweza kuangalia makossa uliyofanya na kujifunza kuwa makini Zaidi kwa kila maamuzi unayofanya kila siku. Kama kuna jambo unalijutia kulifanya au kutokulifanya miaka mitano iliyopita jifunze kwamba miaka mitano ijayo ni hatua gani utaweza kuja kujuta hujazichukua leo?

Angalia mahali ulipo sasa na kule unakotaka kufika kisha uone ni kwa namna gani hasa napaswa kufanya ili uweze kufikia kule unakotaka kwenda. Usiogope kukosea kwani huwezi kujua kama unaweza kama hujakosea. Unapokosea unapata somo kwamba kipi ni sahihi cha kufanya na kipi sio sahihi.

Unapokosea unawapa somo kizazi kijacho kwamba jambo gani hawapaswi kufanya wasije kosea kama wewe.

 

Kuwa Mwanachama Kamili wa Usiishie Njiani Bonyeza hapa.. www.jacobmushi.com/jiandikishe

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. www.jacobmushi.com/vitabu

Jipatie Blog Bora hapa.. www.jacobmushi.com/jipatieblog

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading