Unajua ni kwanini watu hawapati mabadiliko kwenye maisha yao? Au wakianza jambo Fulani baada ya muda mfupi wataacha na kurejea katika hali ile ya kawaida? Inawezekana na wewe ni mmoja wa watu wa aina hiyo unapaswa kutambua kwamba binadamu wanaogopa mabadiliko.
Ndio maana ukitaka kutoka kwenye hali ambayo upo kuna watu wataanza kukupinga na kukukatisha tamaa. Kuna watu wataanza kukwambia kwamba huwezi kwasababu akili zao zinaogopa na kuona haiwezekani.
Inahitaji kujitoa sana na kuweka bidii na juhudi za kutosha ili kuweza kuhama sehemu ulipo kwenda sehemu nyingine. Sio jambo la siku moja ni jambo la muda mrefu na kurudia rudia.
Watu wengi wanaanza biashara na wanakuwa na mawazo makubwa sana na matarajio makubwa lakini wanaishia kukata tamaa pale wanapokutana na ugumu kidogo.
Unatakiwa uelewe kwamba kuna ugumu katika kupata mabadiliko. Kuna kulipa gharama ya kile unachokitaka. Kuna maumivu unatakiwa uyapate ili upate yale makubwa unayotaka. Kama utaogopa maumivu huwezi kupata unachokitaka.
Unatakiwa uelewe kwamba hakuna njia rahisi ya kupata makubwa yeyote unayotaka. Kama ulishaambiwa au umekuwa unafikiri ni rahisi labda kuna mahali unakwenda kujiunga unapata pesa au vile unavyotaka kirahisi embu sahau kuhusu hilo.
Wengi unaowaona wamefikia hatua kubwa za mafanikio kuna hatua mbalimbali walipita hadi kufika walipo sasa hivi. Hakuna mteremko labda ukubali kuwajibika kwa yale unayotaka yatokee maishani mwako.
Hali uliyoizoea inaweza kuwa chanzo cha wewe kutokwenda mbele. Kipato unachokipata sasa hivi kinaweza kuwa sababu ya wewe kutopata kipato kikubwa Zaidi. Usiruhusu hali yako ya kifedha uliyonayo sasa kukukwamisha kupata yale makubwa Zaidi.
Kuwa Mwanachama Kamili wa Usiishie Njiani Bonyeza hapa.. https://jacobmushi.com/jiandikishe/
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. https://jacobmushi.com/patavitabu/
Jipatie Blog Bora hapa.. https://jacobmushi.com/jipatieblog/
Jacob Mushi
USIISHIE NJIANI
“Piga Hatua”