Siku zote ukitaka kujua kama mtu anakuibia mara nyingi huwa tunawawekea mitego mbalimbali. Lakini kuna baadhi ya vitu huhitaji kuweka mitego wala chochote bali unahitaji tu kuondoa umakini kwa pale ambapo unahisi huyu mtu sio mwaminifu.
Ili uweze kujua mtu ni mwaminifu kwako ondoa umakini kwenye lile jambo unalohisi siyo mwaminifu. Unapoondoa umakini unakuwa umempa uhuru wa kufanya anachotaka na ndipo utakuja kugundua kwa matendo yake kwamba sio mwaminifu.
Kama una mpenzi na unahisi sio mwaminifu sehemu ya kwanza ambayo wengi tunakimbilia ni kukagua simu. Mtu akishajua unakagua simu yake moja kwa moja atakuwa makini ili usigundue chochote. Ninaposema uondoe umakini wako simaanishi uache kuwa makini bali umfanye aone kwamba hauko makini na awe huru. Mtu anapokuwa huru na akaona hakuna anemfuatilia ndipo huanza kujiachia kufanya yale ambayo ulikuwa unahisi.
Ukitaka kujua kama kweli mtu ni mwaminifu kwako mwangalie anafanya nini wakati wewe haupo. Kama umemwajiri mtu usipime uaminifu wake kwenye kazi kwa kuangalia anachokifanya wakati ukiwepo. Tenga muda umtazame wakati haupo kazini anafanya kazi kwa namna gani?
Ni rahisi sana mtu kuongea mambo mazuri sana juu yako wakati ukiwepo lakini je ukiwa haupo anasema nini juu yako?
Ni rahisi sana mtu kuonyesha upendo na kukujali wakati unaweza kumpatia kila anachokitaka je anafanya nini wakati huna chochote cha kumfanyia?
Ni rahisi sana mtu kuwa mwaminifu sana wakati akiwa kwenye mahusiano kwasababu tu yupo kwenye mahusiano lakini muulize angekuwa hayupo kwenye mahusiano tabia zake zingekuwa ni njema vilevile?
Unafiki wa kiwango cha juu ni kufanya jambo lolote zuri ili tu watu wakuone lakini ndani yako moyo wako hujamaanisha kufanya jambo lile.
Ukianza kuona wewe kuna mambo unaogopa kufanya kwasababu unahisi Fulani akijua hatakuelewa basi ujue kiwango chako cha uaminifu kimeshaanza kushuka.
Kama umeamua kuwa mwaminifu kuwa mwaminifu hata wakati ule hakuna anaekutazama au anaekuuliza.
Uaminifu wa mtu unapimwa wakati ule ambao hakuna kitu chochote cha kumlazimisha yeye kuwa mwaminifu.
”Kama umependa Makala Hii Usiache Kuweka Maoni yako Hapa chini”
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Jacob Mushi,
Mwandishi, Mjasiriamali, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,
Simu: 0654 726 668,
Instagram: jacobmushi
Facebook: Jacob Mushi Page
Barua pepe: jacob@usiishienjiani.com