HATUA YA 291: Fikra Chanya, Matendo Chanya.

jacobmushi
2 Min Read

Your Positive Action Combined with Positive Thinking Results in Success. – Shiv Khera

Matendo yako chanya yakijumuishwa na mawazo yako chanya yanaleta matokeo kwenye mafanikio. Kama unataka kufanikiwa lazima uzitangatie mambo haya mawili, mawazo chanya na matendo chanya.

Kama utakuwa na mawazo chanya peke yake bila ya matendo huwezi kupata matokeo mazuri ya mafanikio.

Vilevile kama utakuwa na matendo chanya lakini ukawa na mawazo hasi kichwani mwako utapata matokeo ya kushindwa.

Jitengenezee fikra za kukufanya uchukue hatua chanya kwenye ndoto yako.

Ondoa woga,

Ondoa mawazo ya kushindwa,

Ondoa mawazo yote potofu juu ya mafanikio na anza kutegemea matokeo makubwa kwenye yale matendo yako unayofanya kila siku.

Mafanikio yanaanzia ndani kwenye fikra zako mwenyewe.

Matendo chanya.

Matendo yako unayofanya yanatakiwa yaelekee kwenye yale mafanikio unayotaka.

Matendo yako yanatakiwa yasukumwe na nguvu inayotoka ndani yako Zaidi.

Matendo yako yanapaswa kuwa ni kila siku sio leo umefanya kesho umeacha.

Matendo yako yanatakiwa Yazidi sababu za kutokuchukua hatua. Pale unapotakiwa kufanya jambo Fulani lifanye bila ya kuleta sababu nyingine na kuahirisha.

Matendo yako yanatakiwa yaweze kushinda tabia za kuahirisha mambo.

Matendo yako yanatakiwa yaweze kuzidi maneno unayosema.

Matendo yako ndio mafanikio yako. Tenda Zaidi kuliko hata unavyosema kwa watu.

Kila unapochukua hatua amini inawezekana kufanikiwa.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Jacob Mushi,

Author, Entrepreneur, Trainer, Life Coach,

Simu: 0654 726 668/0755192418,

Twitter: jacobmushitz

Instagram: jacobmushi

Facebook: Jacob Mushi Page  

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading