Mara nyingi tumekuwa tukitamani Maisha mazuri sana kwenye akili zetu na kujiambia ipo siku tutafikia Maisha hayo. Mara nyingi hali hii huleta huzuni hasa pale unapowaona watu wa rika lako wanaishi Maisha ya tofauti na mazuri sana kuliko wewe.

Kitu cha muhimu kutambua ni kwamba hauko hapo ulipo sasa kwa bahati mbaya inawezekana ni kwa makosa yako ndio lakini sio sababu ya wewe kutokufurahia hapo ulipo. Ishi Maisha ya sasa kwa usahihi usijisahau ukabaki uanatazama mbele ambako hujafika bado mwisho ukashindwa kuishi na kufurahia Maisha kwenye hatua uliyopo.

Hatua uliyopo sasa ni nzuri sana kama umeweza kusoma maandishi haya upo kwenye hatua nzuri sana. Furahi kwakua unaelekea kwenye ile picha unayoitamani. Unayakaribia yale Maisha ambayo unafikiri ndio mazuri. Lakini usisahau unatakiwa kuishi sasa.

Chochote ambacho kinatakiwa kufanyika sasa hivi kifanye kwa nguvu zote. Kama ni kuonyesha upendo onyesha kwa nguvu zote. Kama ni kuwa karibu na watu unaowapenda wape muda. Huko unakofikir labda ukifika ndio utaanza kuwa karibu na familia yako unaweza usifike na wote au ukafika na muda usitoshe bado.


Tambua majira uliyopo sasa unatakiwa kufanya nini na ukifanye kwa usahihi. Muda haurudi nyuma kuna siku utakuja kujutia muda uliokuwa unapoteza kipindi cha nyuma.

Karibu sana.
Jacob Mushi.
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668
jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading