Kuna wakati mtu anaweza kuja kuomba ushauri halafu akategemea kwamba utampa njia rahisi Zaidi au shortcut ya kutatua changamoto zake. Wakati mwingine unaweza ukapewa njia ngumu Zaidi lakini yenye manufaa kwako wewe mwenyewe.

Kutegemea kupewa njia rahisi ndio kunawafanya wengi waache kufanya vitu sahihi na mwishoe kupotea. Kama utategemea upewe muujiza wa kutatua changamoto yako Rafiki yangu utakuwa unapotea ni bora ungeenda kwenye maombi ukaombewa halafu ukasubiri majibu.

Ushauri unaopokea unaweza kuwa mgumu Zaidi ili kupima ni kwa jinsi gani umejitoa kwenye kila unachokitaka.

Ushauri unaweza kuwa mgumu Zaidi ili kupima nidhamu yako.

Ushauri unaweza kuwa mgumu Zaidi ili upate funzo kwenye kile ambacho unatakiwa kufanya.

Hakuna ambacho utakifanya halafu kisiwe na matokeo chanya kwenye Maisha yako. Wengi wanatafuta vitu virahisi lakini wanasahau kuangalia pia thamani ya kile wanachokichagua. Unaweza kufanya kitu kirahisi lakini ikakuchukua muda mrefu sana kutimiza kile unachokitaka.

Unaweza kufanya kitu kigumu ukajikuta umejifunza jambo ambalo litakusaidia kwenye Maisha yako yote. Yaani kila uendako lile somo ulilopata unakuwa unalitumia. Mfano unaweza kujifunza kunyenyekea, kuongea na watu, kuwashawishi wateja wako wanunue, na mengine mengi kulingana na ushauri ambao umeupokea.

Kama ni kweli umedhamiria kufanya utatafuta njia na wala hutakuja na sababu za kwanini huwezi kufanya kile unachokitaka. Utaacha kuendelea kusubiri siku moja ambayo huifanyii kazi.

 

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp… https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading