Imani ndio inaweza kuamua matendo ya mtu juu ya kile unachokifanya. 

Huwezi kufanya jambo kwa ujasiri na kujiamini kama huna imani nalo.

Imani inazidi uwezo ulio nao. Unaweza kuwa na uwezo mkubwa sana lakini kama huna imani ya kufanikiwa kwenye jambo unalolifanya utajikuta unashindwa kila wakati.

Kuna vitu vingine unashindwa sio kwasababu hujui au una bahati mbaya ila ni kwasababu imani yako ni ndogo sana.

Ongeza imani yako kwenye kazi, na kwenye kile unachokifanya kila siku. Amini kwamba unakwenda kufanikiwa.
Unapokuwa na wasiwasi ndio mwanzo wa kufanya kwa viwango vya chini.

Kile unachofikiri ndani yako kinaletwa na imani yako. Kile unachofikiri ni muhimu sana kuliko unachokifanya. Kama utakuwa na fikra potofu hata uwe na juhudi kiasi gani bado utakuwa unakwama kila wakati.

Tengeneza imani yako. Wako watu walikuwa na ujuzi mdogo, nguvu chache lakini wana imani kubwa wakaweza kufanya mambo makubwa sana.

Ni mimi Rafiki Yako,
JacoMushi.

#UsiishieNjiani
Piga Hatua Timiza Ndoto Yako

Pata vitabu vya biashara na mafanikio hapa www.jacobmushi.com/patavitabu

Jipatie Blog na Utengeneze Kipato www.jacobmushi.com/jipatieblog

Jiunge na Kundi Maalum la WhatsApp www.jacobmushi.com/whatsapp

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading