Unaweza kujivunia cheo, unaweza kujivunia mali nyingi ulizonazo, unaweza kujivunia sura yako nzuri sana, unaweza pia kujivunia umbo lako zuri linalovutia lakini naweza kukwambia hivyo vyoote sio vitu vya kujivunia.
Unacho kitu kimoja ambacho unaweza kujivunia kitu hiki ni ile zawadi ambayo Mungu ameweka ndani yako. Zawadi hiyo Mungu ameweka ili uitumie kuwahudumia wengine. Hichi ndio kitu ambacho unaweza kusimama na kusema najivunia kutambua zawadi iliyopo ndani yangu.
Najivunia kuweza kuifanya dunia kuwa mahali bora pa kuishi Zaidi kuliko nilivyoikuta.

Najivunia kubadili Maisha ya watu wengi kwa kupitia bidhaa zangu, kampuni zangu, au huduma ninayoitoa.

Najivunia kuwa faraja kwa wengi sana hapa duniani.
Kitu ambacho unaweza kujivunia kuwa nacho kiwe kimeleta faida kwa wengine sio faida kwenye Maisha yako binafsi.

Nimekuwa nakutana na watu wengi wanaowaza kufanya vitu kwa faida zao binafsi ndio maana kamwe hawafanikiwi na hata wakifanikiwa basi hawadumu kwenye mafanikio yao.

Maisha haya ya sasa ukijivunia cheo ulichonacho ukasahau kwamba kuna siku kitapotea unajitengenezea shimo baya la kujifukia mwenyewe.

Wako watu wengi sana ambao wanajisahau kabisa kwamba kuna siku watapoteza vyeo hivyo. Wakati mwingine wanatumia kukandamiza wengine.
Kama kuna kitu unatakiwa ujivunie nacho ni kugusa Maisha yaw engine kupitia kile ulichopewa sio kujivunia cheo au madaraka Fulani.

Karibu Sana.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading