HATUA YA 335: Hamasa Yako ya Ndani Inaletwa na Nini?

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read

Kila mtu kulingana na kile anachokitaka kuna namna anakuwa na hamasa ndani yake. Swali la kujiuliza ni kitu gani hasa kinakupa hamasa? Kitakachoamua udumu kwenye maamuzi uliyofanya ni kile chanzo cha hamasa yako.

Kitakachoamua uweze kushinda changamoto ni kile chanzo cha hamasa yako ya ndani. Kama ndani yako hakuna kitu kinachokusukuma kufanya kama vile vya nje lazima kuna mahali utakwama. Kukosa hamasa ya ndani ni kama umeamua kufanya jambo kwa kuiga wengine.

Hamasa ya ndani inatakiwa iletwe na maono yako. Kule ambapo unapaona, kule ambapo unataka kufika siku moja ndio kunatakiwa kuwe hamasa yako kubwa. Japokuwa kuna watu wengi sana wanaweza kukuhamasisha hamasa zao zinaweza kupotea haraka sana ila hamasa ya ndani ndio inadumu.

Kuwa makini na msukumo wako wa kufanya maamuzi. Ukiwa na msukumu wenye kusudi baya ni lazima utashindwa. Kama unasukumwa na maumivu ambayo ulishawahi kufanyiwa ni rahisi sana kukosea au kufika mahali ukaona yote uliyofanya hayana maana.

Maono ndio yanatakiwa yawe msingi mkuu wa Maisha yako. Kila maamuzi unayofanya yawe yanaongozwa na maono yako. Ukiona unafanya maamuzi yaliyo nje ya maono yako ujue huwezi kufika mbali.

Usikubali kufanya maamuzi hata kama jambo ni zuri kiasi gani kama halikupeleki kule unapotaka kwenda. Kama halina mchango wowote wa kujenga maono yako achana nalo maana unakuwa unapoteza muda.

Wako watu wamepotea kwasababu ya kufanya maamuzi kwa kuwaangalia wengine badala ya kuyatazama maono yao. Kule unapotaka kwenda ni kwa muhimu Zaidi kuliko kitu kingine chochote.

Ongozwa na Maono Yako Kwenye Kila Maamuzi.

 

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp… https://jacobmushi.com/whatsapp/

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading