Imani huja kwa kusikia, tunasikia vitu vingi sana tunavyovihitaji na tusivyovihitaji kabisa kwenye maisha yetu.
Kile unachokipa nafasi ya kukisikia zaidi kinajenga imani ndani yako.
Kama unafuatilia kufanikiwa, unasikiliza na kusoma mafundisho ya mafanikio unajenga imani katika Mafanikio.
Kama utawekeza muda wako katika kufuatilia bahati nasibu, kubeti, kufanikiwa kwa ghafla na imani yako itajengwa huko.
Cha ajabu ni kwamba sio kila imani inaleta matokeo ya kweli. Ukiamini Kwamba utakuja kufanikiwa siku moja na huku hakuna unachokifanya basi ujue imani yako imekufa.
Imani inafuatana na matendo. Imani mbovu inafuatana na matendo, imani potofu inafuatana na matendo.
Kama Unataka kuishi maisha ya tabu hapa duniani ni ujenge imani yako katika bahati. Wengi wanaoamini katika bahati hawana kitu wanafanya wanaishia kusema ipo siku tu.
Usitegemee mavuno kwenye shamba ambalo hujalipanda. Lazima ukubali kulipa gharama ya ile imani yako. Imani yenye matendo.
Unaamini utafanikiwa ndio lakini ni lazima uwe na kitu unachokifanya ambacho kitakupeleka kwenye mafanikio.
Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi
#UsiishieNjiani
“Chukua Hatua, Timiza Ndoto Yako.”
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog
Karibu Usiishie Njiani Academy https://jacobmushi.com/whatsapp/