HATUA YA 354: Usijipe Tafsiri ya Mabaya.

jacobmushi
3 Min Read

Unaweza kupitia hali mbaya muda mrefu kwenye Maisha yako hadi ukaanza kujiona wewe ni yule mtu ambaye anapitia hali mbaya.

Unaweza kuwa umeshindwa kudumu kwenye mahusiano na watu mbalimbali kiasi kwamba ukaanza kujiona wewe ndio uko hivyo yaani wewe haukaagi kwenye mahusiano muda mrefu.

Inawezekana pia hadi sasa umeshafanya biashara nyingi na zote zimefeli yaani hakuna iliyokuletea faida ya kuonekana. Umefikia Hatua ya kusema kwamba biashara haikufai wewe bora ukatafute ajira tu.

Inawezekana pia umeishi Maisha ambayo hayana amani hata kidogo wewe kila siku ni kugombana na kutokuelewana na watu. Umefikia mahali unataka kusema wewe ndio uko hivyo.

Leo nataka nikwambie haijalishi hali mbaya yeyote unayopitia. Haijalishi tatizo limejirudia kiasi gani kwenye Maisha yako, wewe sio tafsiri ya mambo mabaya yanayoendelea Maishani mwako.

Bila kujali umeshindwa kudumu kwenye mahusiano muda mrefu kiasi gani bado haimaanishi hutadumu tena. Kama ulianzisha biashara ukashindwa haimaanishi utashindwa kila wakati. Kama umekuwa ni mtu wa kupata hasara kwenye kila unachokigusa haimaanishi wewe ni mtu wa mikosi.

Kila hali mbaya iliyopo maishani mwako inaweza kuondoka na ukawa mtu mpya. Kinachofanya uendelee kurudia makossa yale yale ni kwamba umejitengenezea hofu ndani yako kutokana na kwamba ulishawahi kushindwa hapo mwanzo.

Akili yako umeiambia kwamba wewe huwa unashindwaga kila ukifanya biashara. Umeiambia akili yako kwamba wewe haudumugi kwenye mahusiano Zaidi ya miezi sita. Hivyo basi akili yako (kwa kiingereza ni subconscious mind) inakuletea matokeo ya kile ulichoiambia.

Ukitaka kubadili hali mambo mabaya yanayojirudia kwenye Maisha yako lazima uanze kubadili ndani ya akili yako (subconscious mind). Lazima uondoa mfumo wa kushindwa uliojitengeneza wenyewe kwasababu ya kurudia rudia kwa kushindwa au kufeli.

Siku zote anza na akili yako, itibu akili yako kwanza. Tatizo lipo ndani yako achana na matokeo ya kushindwa. Achana na matokeo ya kuachwa na mpenzi. Achana na matokeo ya kupata hasara kwenye biashara. Shughulika na akili yako, kuna formula mbovu ambazo umezitengeneza ndio zinakuletea matokeo mabovu.

Ukiweza kutengeneza formula sahihi kwenye akili yako basi matokeo ya chochote unachokifanya yatakuwa sahihi.

ILI UWEZE KUTENGENEZA FORMULA SAHIHI KWENYE AKILI YAKO JIUNGE NA USIISHIE NJIANI ACADEMY.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Chukua Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Usiishie Njiani Academy https://jacobmushi.com/whatsapp/

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading