Kumekuwa na watu wengi ambao wanaweza kuona makossa na matatizo juu ya vitu lakini ni wachache wanaweza kuchukua hatua na kuleta suluhisho. Badala yake wanabaki wakilalamika kwa kusema ingekuwa hivi ingekuwa vile… kama wewe umeweza kuona chochote hakipo sawa basi ujue hiyo ni fursa kwako kuleta mabadiliko mahali pale.
Kama umeona kuna watu wanafanya kitu Fulani vibaya acha kuwaongelea ooh watu Fulani hhawafanyi kitu Fulani vizuri. Badala yake wewe ingia kwenye hicho kitu na ukifanye vile ambavyo unaona ndio inatakiwa kufanyika. Acha Maneno mengi sana chukua Hatua t umara moja matokeo yaje tuone kama kweli ulichokuwa unakiongea unakiweza au unajua tu kukosoa.
Kile ambacho unakilalamikia sana basi wewe ndie unatakiwa ulete suluhisho. Kama umeweza kuona makossa ya kitu maana yake una majibu ya lile kosa, badala ya kuendelea kulalamika unachotakiwa kufanya ni kuleta suluhisho.
Usipoteze muda kuendelea kulalamika kwasababu hakuleti matokeo yeyote. Umeona sehemu kuna vumbi sana badala ya kulalamika na kusema hapa hapamwagi maji nenda kamwage wewe.
Kwenye jamii yako umeona maadili yamevurugika badala ya kukaa na kuongea tu na kuendelea kusema Vijana wameharibika inuke nenda kawafundishe.
Kama unaona kwenye dini yako kuna mambo hayafundishwi tena acha kulalamika nenda kafundishe.
Kama unaona kuna mahali penye udhaifu na hakuna wengine wameuona maana yake wewe ndie unatakiwa ulete suluhisho mahali hapo. Usiendelee kusubiri mwingine achukue Hatua wakati wewe ndiye ulliyeoneshwa tatizo.
Ukiweza kuna tatizo maana yake unaweza kuja na suluhisho. Usibakie kulalamika nenda Hatua ya ziada uje na suluhisho ya kile ambacho umekuwa unaona hakifanywi vizuri.
Rafiki yangu chochote unachokiona kinafanywa vibaya basi hiyo ni fursa kwako kwenda kukifanya vizuri na kuleta mabadiliko yale unayoyataka. Wewe ndio mabadadiliko yale ambayo unayoyataka.
Rafiki Yako,
Jacob Mushi