Habari Rafiki yangu, zimepita siku chache kidogo sijakuandikia Makala katika Mtandao wetu. Najua umekuwa unatamani sana kunisoma lakini haikuwa katika uwezo wangu kukuandikia kwa wakati huo. Nimerudi tena, ninaendelea kuandika, ninaendelea kuzungumza na wewe. Sijaacha kuzungumza na watu nilikuwa najaribu kitu kingine cha tofauti ili nione matokeo yake.

Halafu Rafiki yangu najua unatumia mitandao ya kijamii sasa kama upo Instagram naomba unifuate ninaweka nukuu fupi fupi asubuhi na jioni ambazo zinabadilisha Maisha ya watu wengi sana. Sitaki na wewe nikuache nyuma kabisa ungana na wenzako hapa.. https://www.instagram.com/jacobmushi/  bonyeza Maneno hayo utakwenda moja kwa moja kwenye ukurasa wangu ama unaweza kunitafuta kwa jina @jacobmushi.

Jana katika kutafakari kwangu sana kuhusu Maisha nikajikuta nawaza sana juu ya kilimo. Unajua Maisha yetu ni sawa na mtu anaefanya kilimo cha msimu au kilimo cha mazao ya muda mfupi. Hii ni kwasababu sisi binafsi hatudumu hapa duniani ila kwa yale ambayo tumeyafanya ndio yanaweza kudumu hapa miaka mingi Zaidi.

Unajua pamoja na wewe kufurahia sana chakula kitamu ambacho umekula ni kwasababu kuna wakulima ambao hawajakata tamaa kuendelea kulima pamoja na hasara Nyingi ambazo wamekuwa wanapitia. Wangekata tamaa labda tungekuwa na uhaba wa chakula na vingepanda bei sana. Sasa na wewe kile ambacho unakifanya kabla hujakata tamaa watazame wale watu ambao unawahudumia, embu yaone Maisha yao yanakwenda kuwaje endapo wewe utaacha kufanya kile unachokifanya?

Mimi kuna nyakati huwa nakuwa kama nimechoka hivi kuandika lakini ninaweza kupokea simu au ujumbe kutoka kwa mtu mmoja ambaye amesoma Makala ikamgusa na kumvusha Hatua nikajikuta Napata nguvu mpya. Sasa siku nyingine nikijikuta nakata tamaa nawafikiria watu ambao Maisha yao bado ni magumu kwasababu tu hawajasikia au kusoma Makala na Vitabu vyangu. Najikuta natamani kuendelea tu kwasababu kuna Maisha ya wengi yanahitaji maarifa.

Kuna Maisha ya wengi ni mabovu yanahitaji kile ambacho unakifanya. Unapokata tamaa maana yake unakuwa umewatelekeza watu wengi ambao umeitwa kuja kuwahudumia hapa duniani. Ndugu yangu wewe ni sawa na mkulima watu wanategemea chakula unacholima ili Maisha yao yaweze kusonga mbele. Usikatishwe tamaa na ugumu kwasababu kama msimu huu umekuwa mbaya basi msimu unaofuata utakuwa bora Zaidi.

Nataka nikutie moyo sana ile biashara unayofanya inawasaidia watu. Ile kazi unayofanya inawasaidia watu wengi. Kama tu unaona kuna Maisha ya watu yanakuwa magumu kwasababu yako basi iache lakini kama kuna watu unawasaidia kwa kazi endelea kwa bidii sana.

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

https://jacobmushi.com/huduma/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading