Angalia kile watu wengi wanafanya kisha wewe fanya kinyume na wao na utaweza kuwa na mafanikio makubwa. Kama watu wengi hawaamki mapema basi wewe amka mapema kuliko mtu mwingine yeyote.

Kama watu wanakuwa bize na simu zao kwenye magari wewe kuwa bize ukisoma kitabu au Makala kama hizi ambazo zitakufanya uwe bora Zaidi.

Kama watu wengi wanafanya biashara kwa mfumo wa kawaida ambao umezoeleka basi wewe nenda kinyume nao fanya tofauti uone matokeo makubwa.

Watu wengi wanatumia muda mwingi kufanya vitu ambavyo vinawaletea raha ya muda mfupi na kujikuta wanasahau kwamba kuna mambo ambayo ni ya muhimu sana kufanya. Yale mambo ya muhimu sana na yenye matokeo makubwa sio marahisi hata kidogo, yanahitaji ujasiri wa pekee na nguvu isiyo ya kawaida ili uyafanye.

Ukikubali kwenda tofauti na wengi wanavyokwenda basi wewe utakuwa umejiweka sehemu ambayo kila mtu atatamani kuja hapo lakini hajui umefikaje. Kama ni biashara ukiweza kuifanya kwa namna ya tofauti utajitofautisha na wenzako Wateja wataambiana pale kwa Fulani ukienda unahudumiwa vizuri, unapewa hiki na kile na mwisho wake utafika viwango vya juu vya mafanikio.

Chagua kuwa wa tofauti, jitenge na kundi, usifuate mkumbo.

Kitu cha ajabu ni kwamba ili uwe wa tofauti unapaswa kufanya vitu ambavyo vinaonekana ni vidogo vidogo sana lakini vinaleta matokeo makubwa.

Usikubali kuwa kama wengi kwasababu matokeo yake ni ya kawaida, chochote kinachotumiwa na kila mtu kinakuwa kitu cha kawaida sana.

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

https://jacobmushi.com/huduma/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading