Kipaumbele kikubwa kwenye Maisha yako ni kipi? Ndugu yangu kama huna kipaumbele kikuu cha Maisha ambacho ndio kinakuwa sababu ya wewe kuamka mapema, kufanya kazi kwa bidii utakuwa unapoteza muda. Lazima Rafiki uwe una kitu cha muhimu la sivyo Maisha yako yatakuwa ni dharura tu. Usiishi Maisha ya kufanyia kazi vitu vya dharura vinavyotokea kwenye ishi kwa kufanyia kazi vipaumbele vyako.

Kama ukikosa vipaumbele watu wenye vipaumbele vyao watakuwa wanachukua muda wako, watachukua nguvu zako. Watatumia fedha zako kwasababu hujui ni wapi hasa pa kutumia fedha kwasababu hujaweka vipaumbele.

Lijue kusudi la wewe kuwepo hapa duniani, jua hasa ni kitu gani unakitaka hapa duniani, ni wapi unataka kufika. Fanya hivyo ndio vipaumbele hakikisha unafanya kila namna ili uweze kutimiza.

Ukiwa unasafiri akili yako inakuwa inawaza kitu kimoja tu yaani kusafiri. Na kwasababu hakunaga uwezekano wa kurudishiwa nauli yako engapo utachelewa na kuachwa na gari basi linakuwa ndio jambo la muhimu kuliko vyote.

Kukiwa na kikwazo cha aina yeyote mbele yako utatumia njia yeyote ile ili usonge mbele ufike stendi. Kitu cha ajabu ni kwenye malengo yako na Maisha yako, unapanga vitu unaihirisha. Unasema utaamka mapema usome Vitabu huamki mapema.

Unasema utachukua Hatua Fulani lakini huchukui tena. Naomba nikwambie endapo ukiyachukulia Maisha yako kama siku ya safari basi hakuna kitakachoshindikana. Utatafuta njia ya aina yeyote ile ili utimize kile ulichokipanga.

Malengo yako sio kitu cha kusema utafanya siku nyingine, kuwa mtu ambaye ukisema wiki hii nafanya kitu hiki unafanya na kinatokea kweli. Ukisema unataka kukutana na mtu Fulani unafanya kila linalowezekana ili uweze kukutana nae.

Acha kuyachukulia Maisha yako kirahisi Rafiki yangu.

Jacob Mushi

https://jacobmushi.com/huduma/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading