HATUA YA 53: Madhara ya Kukaa na Watu Hasi.

jacobmushi
By jacobmushi
3 Min Read

Watu Wanofikiri Hasi kwenye Maisha, mara nyingi hukosoa au kutoa sababu ambazo zinawatetea pale walipo.

Watu Hasi wanaweza kuwa sababu ya wewe kutokwenda mbele kwenye mafanikio. Jana jioni nilipita mahali nikasikia watu wakizungumza juu ya mtu Fulani maarufu na mwenye pesa, watu wale walikuwa wanasema ooh! Mnamwona Fulani ni tajiri? Huyu alitoa kafara ndio maana kafika pale alipo!

Mara nyingi watu hasi huwaza hasi kwenye mafanikio ya wenzao. Watu hasi ukiwaeleza ndoto yako kubwa wataanza kukuelezea ni jinsi gani haiwezekani.

Watu hasi wamechoka na Maisha na wameyakubali Maisha wanayoyaishi na hawataki kutoka hapo walipo.

Watu hasi ni sawa na kuku ambaye ameshakubali kwamba yeye ni wa chini siku zote. Akiona tai wanaruka anasema yule mbawa zake ni kubwa kuliko zangu.  Akiona tai wanaruka juu anasema mimi ni kuku tu siwezi kuruka. Hivyo unapojichanganya na watu kama hawa uwe makini na vitu unavyowaambia wanaweza kukuingizia sumu kwenye akili yako.

Kuna maneno wanaweza kuyasema ukayachukulia ya kawaida sana lakini yakakuingia na kukufanya ukashindwa kusonga mbele.

Mfano ukiwa kwenye mahusiano ukamfata mtu mwenye fikra hasi ukamwelezea juu ya tatizo Fulani kwenye mahusiano yako anaweza kukushauri achana na huyo mtu! Ukiona ameanza hako katabia ujue ameanza kukusaliti. Kumbe ukweli halisi sio huo.

Mtu hasi akisikia watu Fulani wenye mafanikio atasema wale ni mafisadi, wale wametoa kafara, wale wanauza madawa ya kulevya. Haiwezekani wakawa na pesa nyingi kiasi hicho hawa wameiba tu hawa! Hizi ndio fikra zao mara nyingi. Ukiwa na marafiki kama hawa kwanza utafanana nao, pili hauwezi kuendelea mbele.

Watu hasi ni wakosoaji wa kila kitu kizuri kinachoanza. Mara zote wakikuona unaanza vizuri watasema hufiki mbali.

Watu hasi wapo siku zote kwenye jamii zetu hatuwezi kuwaondoa bali tunachoweza ni kupambana na kutimiza ndoto zetu ili watambue kwamba inawezekana.

Wapende sana watu hasi usiwachukie ila kaa nao mbali. Watu hasi wanaweza kuwa ndugu zako wa karibu, anaweza kuwa baba yako, mama yako au hata kaka yako. Huwezi kuwachukia. Mara nyingi unatakiwa usiwaambie yale mambo yako makubwa sana.

Soma: Mawazo Hasi

Wakati mwingine watu hawa wanakushauri kwamba achana na hizo ndoto sio kwamba ni kwa ubaya ila ni kwasababu ufahamu wao haujafunguka. Hivyo huna haja ya kuwachukia bali wachukulie kana kwamba wako ndani ya chumba chenye giza na hawajawahi kuona mwangaza hivyo wataopa mwangaza wowote.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Jacob Mushi,

Author | Trainer | Entrepreneur

Simu: 0654 726 668 |0755192418,

Twitter:  @jacobmushitz

Instagram: @jacobmushi

Facebook:  Jacob Mushi 

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading