HATUA YA 54: Unamhitaji Mtu Huyu.

jacobmushi
2 Min Read
Tupo kwenye ulimwengu ambao watu wanafanya mambo wenyewe bila kupata mtu wa kuwaongoza hivyo hupelekea watu kukosea.

Vilevile watu hukosa mtu wa kuwashauri wakati wanapopitia magumu  na hivyo hukata tamaa haraka.

Unamhitaji mtu wa kukuonya pale unapokosea.

Unahitaji mtu wa kukuongoza kuelekea kwenye ndoto na maono yako.

Unahitaji mtu ambae anafuatilia kwa karibu kile unachokifanya ili usiharibu.

Mwandishi wa Kitabu cha Rich Dad, Poor Dad ameelezea namna alivyokuwa na baba hawa wawili mmoja akimshauri akaishi maisha ya kutegemea ajira na mwingine akimshauri kufanya biashara.

Kama utamkosa huyu Rich Dad kwenye maisha yako kuna nyakati zitafika utakwama njiani na utakosa mtu wa kukufundisha namna ya kutoka hapo ulipo.

Nyumba yeyote inapojengwa hasa nyumba ya thamani inakuwa na mafundi wanaoijenga na wasimamizi yaani wakaguzi wanaowaongoza mafundi.

Wewe ni fundi wa ndoto yako wewe ndio unaijenga ndoto yako.
Lakini unahitaji mtu wa kukusimamia na kukuongoza ili unapokosea kuweka tofali mahali pasipofaa upate maelekezo.

Huku duniani kuna watu wengi wanakutazama na wanaweza kuja kukupa ushauri wa aina mbalimbali. Kuna ambao unaweza kuchukua na kuna wa kuachana nao.
Lakini kama huna mtu maalumu ambaye unaweza kwenda kwake na kumwelezea unachokifanya utakosa mengi sana.

Soma: Madhara ya Watu Hasi

Tafuta mtu huyu kwa namna yeyote ile umpate.

Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: 0654726668
Email: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading