Mara nyingi tunapitia changamoto mbalimbali kwenye maisha na tunapofikia kwenye hali hizo wengi wetu badala ya kuendelea mbele tunabaki palepale.
Unapojikwaa jifunze kutembea vizuri lakini usikwame kwenye ile sehemu uliyoangukia.
Safari bado inaendelea hivyo kama utabaki unaendelea kutazama kisiki utapoteza muda wako.
Hakuna namna ambayo utaishi bila ya changamoto cha msingi ni kujifunza ili usije kujikwaa sehemu ile ile.
Maisha yako yatasonga mbele kama utakubaliana na hali iliyojitokeza ukajifunza. Na ukasonga mbele zaidi.
Jiulize tu kila unapojikwaa je narudia makosa? Yaani unajikwaa sehemu ile ile kila wakati?
Kama unajikwaa sehemu ile ile kuna tatizo unatakiwa utatue maana yake ni kwamba hausongi mbele umesimama sehemu moja.
Karibu Sana
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: 0654726668
E-mail: jacob@jacobmushi.com
jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading