HATUA YA 79: Huyu Ndiye Mtu wa Muhimu Kuliko Wengine..

jacobmushi
By jacobmushi
3 Min Read
Duniani kuna watu wengi sana bilioni saba lakini kuna mtu mmoja wa muhimu sana kuliko wengine wote. Ni muhimu sana ukamtambua ili aweze kukupa mchango wake wa nguvu kwenye kile unachokifanya.
Ukishindwa kumjua mtu huyu mara nyingi utajikuta unakosa Amani ya moyo kwasababu ndiye anaesikiliza matatizo unayopitia.
Mara nyingi tunakuwa bize sana hadi tunakosa muda wa kukaa naye na kuzungumza naye. Mara nyingine tunawapa watu wengine muda lakini tunamsahau mtu huyu wa muhimu sana kwenye Maisha yetu.
Bila mtu huyu huwezi kufikia mafanikio yeyote. Bila mtu huyu vyote unavyovitafuta hutavifurahia kamwe. Mtu huyu anahitaji kujaliwa kupewa muda, kuzungumza nae mara kwa mara.
Mtu huyu narudia tena ndio anaehutaji muda wako Zaidi ya mtu mwingine yeyote huku duniani. Kama kuna zawadi huwa unaandaa jitahidi uwe unamwandalia.
Inawezekana umeanza kujenga picha mbalimbali za huyu mtu lakini nitakwenda kumtaja muda  si mrefu. Ni mara ngapi unapata muda na marafiki? Ni mara ngapi unapata muda wa kuangalia Tv, kusoma magazeti, na kusikiliza muziki? Jibu linaweza kuwa karibia kila siku.
Lakini mtu huyu umemsahau. Nikikuuliza mara ya mwisho ulimpa muda wako lini itakubidi uanze kufikiria kwanza kwasababu umesahau umuhimu wake.
Ukweli ni Kwamba Bila mtu Wa ndani ambaye ndie nafsi yako huwezi kwenda popote. Ili uweze kufurahia Maisha lazima mtu wa ndani awe na furaha. Kitu cha kushangaza watu wengi tumemsahau mtu huyu. Hatuna muda nae tuko bize na pilika pilika za Maisha.
Leo nataka kukwambia mpe muda mtu huyu wa ndani. Huyu ndio kila kitu kwako. Huyu ndiye amebeba picha kubwa ya Maisha yako ya baadae. Hivyo tenga muda uwe unatafakari pamoja nae na kuzungumza nae.
Hakikisha kila siku unampatia muda angalau nusu saa tu inaweza kutosha. Kaa sehemu tulivu bila chombo chochote cha mawasiliano. Maana yeye anapenda utulivu. Msikilize atakueonyesha mahali unapotakiwa kwenda.
Jijengee tabia hii ili uweze kupata mafanikio makubwa. Vyote unavyovitafuta kama utakosa Amani ya ndani na mtu huyu huwezi kufurahia. Ndio maana tunasikia watu wanajiua na mtukio mengine ya ajabu hii husababishwa na mtu huyu wa ndani kukosa ushirikiano na sisi.
Bora ukose mahusiano na wengine lakini uwe na mahusiano bora na mtu huyu.
Karibu sana.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
2 Comments

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading