Ukweli ni kwamba uthamani wa kitu haupo kwenye bei yake bali upo kwenye matumizi yake. Kama kitu kitakuwa ghali sana halafu hakina matumizi ya maana kwenye maisha yako hakuna haja ya kuwa nacho.
Unaweza usinielewe kabisa kama unashindwa kufikiri vizuri. Gari la tsh milioni mia ni la thamani kubwa kwa yule anaelitumia kwenye matumizi yake. Wewe kwa ngazi uliyopo sasa hivi ya maisha gari hilo ukiwa nalo linaweza kuwa ni anasa. Kama ni anasa basi thamani yake inapotea.
Lazima ujue kuvithaminisha vile vitu ulivyonavyo kutokana na matumizi yake. Unaweza kudhani kwamba wengine wana vitu vya thamani kuliko wewe lakini kumbe wewe ndio una vitu vya thamani kuliko wako.
Mfano rahisi wewe una computer aina ya mpakato (laptop) kampuni ya dell inakutengenezea kipato cha shilingi laki tano kwa mwezi kutokana na matumizi yake. Rafiki yako yeye ana MacBook inayouzwa Milioni 2. Lakini anaitumia kuangalia picha (movie) na kujionyesha kwa watu kwamba ana kitu cha ghali. Kwa kufikiri kwa haraka mwenye kitu cha thamani kuliko mwenzake ni yule mwenye dell. Lakini watu tunaowatazama tutasema mwenye Apple ndio ana computer ya thamani.
Thamani ya kitu inakuja kulingana na matumizi yake. Haijalishi una simu ya ghali kiasi gani kama matumizi yake ni sawa na mtu mwenye simu ya kawaida thamani yake inafanana na ya kawaida.
Kabla hujajiona wewe ni wa chini kwa kutazamam wengine wana nini na weww huna nini tazama kwanza ulivyo navyo vinagusaje maisha yako.
Inawezekana kabisa vile ulivyonavyo vina thamani kuliko kitu kingine chochote.
Jifunze kuvipa vitu thamani wewe mwenyewe kulingana na matumizi yake.
Karibu Sana…
Jipatie Kitabu Kiitwacho Siri 7 Za Kuwa Hai Leo piga 0654726668.
Jiunge Nasi kwenye Group La wasap Kujifunza Zaidi.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: 0654726668
E-mail: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.