HATUA YA 88: Kama Maana ya Mafanikio Kwako Ni Hii Unajidanganya…

jacobmushi
By jacobmushi
3 Min Read
Watu wengi unapozungumzia mafanikio wanajijengea picha Fulani kubwa ya kuifikia huko baadae sana. Lakini wanasahau kwamba baada ya kuifikia hiyo picha ili picha iendelee kuwepo lazima kuna vitu unatakiwa uendelee kufanya.

Wengine wakiambiwa kuhusu Ukijiajiri unakuwa huru wanafikiri uhuru ni kuamua kusafiri popote unapotaka bila ya kuomba ruhusa au kununua chochote unachotaka, pengine kuamka muda unaotaka. Inawezekana na wewe ulikuwa na tafsiri hii kwenye akili yako. Ukweli ni kwamba ulikuwa unajidanganya.

Lazima ujue ni vitu gani vya kufanya kila siku hadi viwe tabia yako kabisa na vikuletee yale matokeo unayoyataka.

Tuchukulie mfano wa mtu anaetaka kutengeneza mwili wake uonekane wa mazoezi na kifua kikubwa. Mtu huyu lazima aamue kufanya mazoezi kila siku au kulingana na ratiba aliyojiwekea hadi lengo lake litimie. Lakini sasa hata lengo likitimia ili aendelee kubakia na mwili ule alioutengeneza lazima aendelee kufanya mazoezi kila wakati.

Kama ataacha mazoezi na kurudia tabia zake za zamani basi moja kwa moja ataharibu mwili wake na ndipo mwili wake utarudia umbo la zamani.
Hivyo ndivyo ilivyo kwenye mafanikio usifikiri labda ukishatimiza ile ndoto yako ndio basi tena unakaa. Ili ubakie na hicho ulichokitafuta lazima ujue ni mambo gani yaliyokufikisha pale na uyafanye kila wakati.


Lazima pia ukubali kuyatazama mabadiliko yanayotokea kila siku ili uweze kusimama sehemu uliyopo.

Watu wengi wamepoteza vitu vyote walivyokuwa wanavitafuta kutokana na tafsiri mbaya juu ya mafanikio.

Kitu Cha Kufanya:
Amua leo ni vitu gani vya kufanya kila siku kwenye Maisha yako. Vitu hivi viendane na kile ulichoamua kukifanyia kazi hadi kitokee yaani maono yako.
Hakikisha unafanya kila siku hadi iwe tabia yako. Kama vile tunavyoswaki kila siku asubuhi ili kuifanya midomo yetu ibakie na harufu nzuri kila siku.

Hili ndio linawafanya watu wenye mafanikio makubwa wanaendelea kubaki huko juu walipofika. Kama ulikua unatafuta siri ya mafanikio ndio hii ya leo niliyokwambia. Wengi huwa wanaanza na kuishia njiani lakini kama ni kweli umedhamiria kuwa au kupata hicho kitu unachokitaka usikubali kukata tamaa.

Tengeneza historia yako mwenyewe kwa kufanya vitu ambavyo wengine wanaishia njiani kila wakati.

Tengeneza ushuhuda wa kuja kuelezea siku moja kwamba ulifanya jambo Fulani hadi likakuletea matokeo.

Kitabu Siri 7 za Kuwa Hai Leo Kinapatikana wasiliana nami kwa 0654726668 kukipata.

Your Partner in Success
Jacob Mushi
Success Motivator, Author & Entrepreneur
Phone: +255 654 726 668
jacobmushi.com
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading