Tuko kwenye zama ambazo kuna vitu vingi sana ambavyo vinaonekana kwama ni vya muhimu sana kuliko vingine lakini havina umuhimu wowote.

Tuna mambo mengi sana ambayo yanaendelea kwenye dunia hii kila siku na yanavutia sana kufuatilia kuliko yale ambayo yanatuhusu.
Kama mtu utashindwa kuwa na nidhamu au kuwa na vipaumbele utajikuta hakuna ulichofanya unapoteza tu siku na Maisha yanaendelea kuwa magumu kwako.
Kama mtu utashindwa kufanya uchaguzi bora wa mambo ya kufutailia ipo siku utaniambia juu ya muda ambao umeshapoteza hapa duniani. Jaribu kukaa chini na utafakari juu ya mambo ambayo yanakuvuta kila siku kufutilia na kujihusisha nayo je ni kweli yana mchango kwenye ndoto yako?
Jaribu kujiuliza leo lengo kuu la Maisha yako wewe ni lipi? Bila kutambua lengo kuu la Maisha utajikuta unavutwa na kila kizuri kinachokuja.
Kuna mitandao ya kijamii inavuta sana watu wengi hadi wanashindwa kufanya kazi kwa ufanisi. Unakuta mtu kila baada ya dakika kadhaa amechungulia kwenye hii mitandao. Unamuita mtu kwenye kikao kila saa yeye anafungua simu.
Kuna habari mbalimbali zinazoendelea hapa duniani kila siku. Ukiangalia kwa makini unakuja kugundua ni matukio Fulani ambayo yanajitokeza kila wakati na hayana mchango wowote kwenye Maisha yako hata kama ukiyajua vizuri sana.
Kama ulikua hujajua kila siku kuna jambo jipya linakuja ambalo linavutia sana kufuatilia kuliko mengine yaliyopita. Kila siku kuna upepo unavuma hakikisha unajua unavua sehemu gani maana usipojua kila upepo utakuchukua.

Wapo watu wa muhimu wanatuhitaji kila siku kwenye Maisha yetu lakini wanatukosa kwasababu ya vitu hivi vinavyochukua umakini wetu kila saa. Watoto, wenzi wetu, wachumba, ndugu zetu wa karibu, maono yako yanakuhitaji kila siku, wewe mwenyewe unahitaji uwe na muda wa kukaa peke yako kila wakati.  Kutokana na mambo mengi yanayoendelea unajikuta unakosa muda kabisa.
Ukifuatilia kila kinachoendelea huku duniani utajikuta unakosa ubunifu kwenye kazi yako. Utakosa uvumbuzi mpya kwenye lile unalolifanya. Fuatilia yale ya muhimu tena kwa kiasi ili ujipe muda wa kufanya yale ya muhimu Zaidi.
Kama kila jambo kwako ni la muhimu basi huna jambo lolote la muhimu.

Kwa Blog nzuri ya Kukuingizia Kipato Bonyeza Hapa…

Jiunge Na semina itakayoendeshwa kwa njia ya mtandao Mwezi wa Nne kwa ada ya Tsh, 5000/= tu Tuma majina yako na neon semina kwenye namba 0654726668
Your Partner in Success
Jacob Mushi
Success Motivator, Author & Entrepreneur
Phone: +255 654 726 668
jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading