Unaweza kupoteza vyote lakini huwezi kupoteza uwezo ambao Mungu ameweka ndani yako. Unaweza kupoteza cheti cha chuo lakini uwezo na maarifa yaliyoko kichwani bado yana uwezo wa kukufanikisha.

Kuna wakati unaweza kujiona wewe huna chochote kwenye ulimwengu huu. Ukajishusha thamani kabisa na kujiweka katika kundi la watu wa kawaida sana. Lakini ukasahau ulizaliwa peke yako na mwenye uwezo mkuu sana ndani yako.
Watu hawawezi kuchukua uwezo uliopo ndani yako. Uwezo huo ni sawa na kisu kikali ambacho kinaweza kukata lakini hakiwezi kutumika pasipo mtu wa kukitumia. Akili yako na uwezo wako mkubwa usipoutumia hauwezi kujitumia wenyewe.
Haijalishi hata kama utapoteza kila ulichonacho sasa hivi kama akili uliyotafutia bado unayo inawezekana kurudisha Zaidi ya ulivyokuwa navyo mwanzo.
Acha kulalamika fanya kitu watu wakione ndio hatua ya kwanza yaw ewe kusonga mbele. Ule msemo wa mwenye nacho ataongezewa ndipo unatumika hapo. Mtu hawezi kukukopea pesa ukafanye kitu ambacho hakionekani, atakuona unataka kumtapeli.
Kama hakuna kitu ambacho kinakutambulisha wewe ni nani na unaelekea wapi kwa hapa duniani basi unapoteza muda amua kuanza sasa. Angalia ni kitu gani kipo ndani ya moyo wako na kinakupa shauku ya kukitimiza siku moja.

Chukua hatua ndogo ndogo hadi ufike pale unapotamani kufika. Hatua mia moja huanza na hatua moja. Usidharau hatua ndogo ndogo unazopiga kila siku zinakupeleka kwenye ukuu.
Usipoamua kuanza sasa hautakaa utoke hapo ulipo sasa hivi.
Chochote unachokianza anza kutengeneza picha kubwa ambayo unataka kuifkia kwenye siku za mbeleni. Fanyia kazi ile picha kubwa hadi itimie. 


Chagua namna gani ambavyo utaanza kutimiza hiyo picha kubwa ndani yako.

Jipatie Vittabu Vya Sauti hapa

Jiunge na semina kwa  njia ya Mtandao tuma majina yako kwennda nambari 0654726668

Jipatie Kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo kwa Tsh elfu kumi tu (10,000) wasiliana nami kwa 0654726668.
Your Partner in Success
Jacob Mushi
Success Motivator, Author & Entrepreneur
Phone: +255 654 726 668
jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading