HATUA YA 98: Kubali Kujinyima…

By | March 22, 2017

Wakati mwingine mafanikio huwa hayaji hivi hivi. Lazima ukubali kufanya vitu vya tofauti..  

Lazima ukubali kujinyima baadhi ya vutu vinavyoweza kuwa sababu ya wewe kurudia hali ya zamani.
Huwezi kuniambia aina ya maisha unayoishi sasa hivi yanaweza kuwa mwanzo.

Jinyime starehe zisizo na lazima. Kaa mbali na watu ambao hukufanya utumie pesa ambazo hukupanga.

Jinyime kukaa na watu ambao hawasomi vitabu. Kaa mbali na watu wasiosoma vitabu, watakuambukiza ujinga wao.

Ulishawahi kukutana na mtu anasema “yaani nafurahi sana kukutana na wewe sijui ulikuwa wapi siku zote” ukiona hivyo ujue mtu huyu alikua anapoteza muda na watu asiowahitaji. Kuna siku utakuja kuujutia muda wako unaoupoteza sasa hivi.

Kuna vitu vingi sana vya kujinyima. Maana umaskini unaletwa kwa kufanya vitu vingi visivyo na ongezeko chanya kwenye maisha.

Jacob Mushi
Author & Entrepreneur

One thought on “HATUA YA 98: Kubali Kujinyima…

  1. Pingback: HATUA YA 99: Kitu Gani Kinakutambulisha? | Jacob Mushi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *