#Ni kweli Maisha hayajawahi kuwa marahisi ila kuna sehemu unaweza kuwa unazidisha ugumu wewe mwenyewe.

“Pale ambapo wewe ni Mjinga Ndipo Wengine Wanakufaidi”

#Ni kweli huwezi kujua kila kitu na ndio maana kwa vile vitu ambavyo huvijui lazima ulipie gharama za kujua. Bahati mbaya sana wengi tunashindwa kutambua ni vitu gani hasa tunavihitaji na kujikuta tunakazana kutafuta vile ambavyo wala hatuvihitaji sana.

#Ni hatari sana kama unamiliki simu ya milioni 3 halafu huna biashara yeyote unayomiliki. Au kama sio biashara basi huna kipato ambacho kinazidi bei ya simu yako kwa mwezi. Sio vibaya kumiliki simu ya ghali ubaya upo pale ambapo wewe unalalamika hali ngumu Maisha hayafai na mengine ya ajabu.

#Inashangaza kumkuta kijana anapenda udaku kuliko mambo yenye maana yeye muda wote yupo bize na habari ambazo hakuna kinachoongezeka kwenye Maisha yake. Lazima Maisha yawe magumu kama hujaupa ubongo wako kazi ya kufikiri. Kama hujaamua kujishughulisha na mambo yanayoongeza thamani yako lazima utaongeza ugumu wa Maisha yako mwenyewe.

#Ni kawaida sana ya watu kupenda vitu virahisi bahati mbaya ni kwamba ukitaka Maisha yako yawe magumu chagua kufanya vitu virahisi. Yale magumu unayoacha ndio unayafanya yatengenezee Maisha yako ugumu Zaidi.

#Lile usilolifahamu ndio unalilipia gharama. Maisha yako yataendelea kuwa magumu Zaidi kama utakataa kujifunza na kuendelea kubeza watu wanaofanya kazi ya kufundisha na kuandaa semina na kwa ajili yako.

#Usikubali kuyafanya Maisha yako yawe magumu Zaidi. Ni vizuri ukajua kwa sasa wakati unapambana ni vitu gani ni vya muhimu Zaidi na vingine ni anasa. Anasa ni vile vitu ambavyo hujafikia uwezo wa kumiliki lakini wewe ukakimbilia kumiliki. Kukopa pesa na kununua gari hiyo ni anasa, kumiliki biashara inayokuingizia kipato na kikakutosha ukajinunulia gari lako haiwezi kuwa anasa.

#kama huna vipaumbele lazima Maisha yako Yazidi kuwa magumu. Kama huna ratiba ya Maisha yako lazima uzidishe ugumu kwenye Maisha. Kama huna utaratibu wa Maisha lazima ugumu uongezeke. Jua ni vitu gani umevisababisha wewe na vile ambavyo huwa vipo siku zote.

 

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Chukua Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Usiishie Njiani Academy https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading