Pamoja na sababu nyingi ambazo zinasababisha wewe kuendelea kubaki hapo ulipo, unapofikiri kwamba wewe huna ndugu wa kukusaidia, huna mtaji wa kutosha kuanza biashara, mazingira uliyopo ni magumu, na sababu nyingine nyingi unazojitetea unakuwa unaziba akili yako.

Pale tu unapoambiwa kwanini huna fedha za kutosha ukaanza kuwa na sababu kede kede unaifanya akili yako iwe zembe ikubaliane na sababu zako kwamba hakuna mtu wa kukusaidia hivyo na akili nayo inalala inasubiri mtu wa kukusaidia.

Unapokuwa mtu wa sababu unakuwa hujaitendea haki akili yako na uwezo wako wa kufikiri kwasababu kama kulikuwa hakuna njia ya kukutoa hapo ulipo hasa katika zile ulizokuwa unazitegemea unatakiwa uiache akili yako itafute suluhisho jingine.

Unaweza kumkuta mtu amezungukwa na fursa nyingi sana lakini ukimuuliza kwanini hana maendeleo anakupa sababu za ajabu ambazo hazina hata msingi.

UNAPOKUWA MTU WA SABABU UNAIPA AKILI YAKO UKOMO WA KUFIKIRI. USIKUBALI KUINYIMA AKILI YAKO HAKI YAKE YA KUFIKIRI. Akili yako ndio inatakiwa ikupe majibu hasa pale mazingira ya kawaida yanapokuwa yameshidnwa kukupa majibu.

Soma: Mambo 5 niliyojifunza Leo

Kila shida unayopitia kwenye Maisha yako ina majibu yake kwenye akili yako. Mungu alikuumba ukiwa kamili kwenye akili yako. Hata kama huna viungo vyote vya mwili embu ipe nafasi akili yako ya kutafuta suluhisho.

Hua napenda kutoa mfano kwamba kama umepelekwa katika mji ambao hujawahi kuishi kabisa huna mtu yeyote unaemjua, huna pa kulala, huna pa kula, utatumia njia gani ili tu Maisha yaweze kuanza kusogea? Huna mtu wa kumpigia simu umwambie mambo yamekwama akusaidie pesa kidogo kama ulivyozoea. Utatumia njia gani ili tu uishi?

Kwasababu sasa hivi kuna mahali unategemea kupata yale mahitaji ya muhimu ndio maana akili yako imelemaa. Ile siku hicho unachokitegemea kitakaposhindwa kukusaidia tena ndio akili yako itaanza kufanya kazi sawasawa. Sasa usisubiri hadi ufikie hapo itumie akili yako vizuri.

USIKUBALI KUJITETEA UKAINYIMA AKILI YAKO HAKI YAKE YA KUTAFUTA SULUHISHO. USIJIPE UKOMO WA KUFIKIRI KWASABABU UNAZOTOA.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi,

Author, Entrepreneur, Trainer, Life Coach,

Simu: 0654 726 668,

Twitter: jacobmushitz

Instagram: jacobmushi

Facebook: Jacob Mushi Page  

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

 

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading