Jinsi Ambavyo Kuchelewa Kufanya Maamuzi Kunavyoweza Kukuongezea Ugumu Wa Kufanya Maamuzi.

jacobmushi
By jacobmushi
4 Min Read
Katika mambo ambayo yanaweza kuwa sababu ya kila mtu mwenye mafanikio kufika pale alipo ni tabia hii ya kufanya maamuzi kwa wakati. Kama umeambiwa tafiti zinasema mwaka huu mvua hazitanyesha nyingi hivyo watu wapande mazao yanayovumilia mvua. Halafu wewe ukakazana kubaki unasubiria mvua ndugu yangu utakosa vyote au ukija kufanya maamuzi utakosa kiwango ulichopaswa kuvuna kama ungewahi kuchukua hatua.



Ukiwa na umri chini ya miaka 18 unakuwa chini ya wazazi na maamuzi yako yanategemea Zaidi nguvu kutoka kwa wazazi. Kuna mambo ambayo ukiamua wazazi watakwambia hapana subiri kwanza.

Ukiwa na umri wa utu uzima au tunaweza kusema ukiwa kwenye familia yako yaani wewe ni baba au mama wa watoto wako. Kuna maamuzi huwezi kufanya peke yako lazima umshirikishe mwenzako la sivyo utakuwa umezua ugomvi kati yenu. Vile vile maamuzi yeyote lazima yawe yanawatazama watoto wenu. Mfano mnataka kuhama mkoa halafu tayari watoto wapo shule wanasoma maamuzi haya yatakuwa ni magumu kidogo kufanyika tofauti na kijana ambaye hajaoa wala hajafungwa na chochote.
Sehemu ambayo inakupasa uitazame kwa umakini ni ujana wako. Kwenye ujana ndipo makossa mengi yamefanywa na kusababisha watu kuwa na Maisha ambayo hawayataki kabisa. Kwenye ujana ndio mtu anakuwa na nafasi ya kufanya maamuzi mengi sana kuliko sehemu nyingine yeyote.

Kama wewe ni kijana unapaswa kuyatambua majira na nyakati ulizopo ndio nyakati za wewe kufanya mambo yatakayobadili Maisha yako. Kuna maamuzi ukichelewa kuyafanya yanazidi kuwa magumu Zaidi.

Lazima ujifunze kuyajua majira na nyakati za Maisha yako. Pia ujue ni jambo gani la kufanya sasa hivi na lipi linapaswa kusubiri. Ukiwa na familia halafu ukapata pesa mahali ambazo hukuzitarajia maamuzi ya kutumia zile pesa lazima yaitazame familia.
Huwezi kuchukua pes azote ukapeleka kwa biashara wakati mnalala njaa nyumbani. Lakini ukiwa kijana huna watu wengi wanaokutegemea hivyo unakuwa na uhuru wa kufanya maamuzi makubwa kwa kile unachokipata.

Kama wewe ni kijana basi angalia sana unayopaswa kuyafanya kwa wakati huu wa ujana na uyafanye. Huko mbele unakoelekea mambo yanaweza kuwa magumu Zaidi maana hutakuwa mwenyewe. Ukiwa na gari na bado hujaoa maamuzi ya kuuza gari unaweza kuyafanya ukiwa njiani unatembea au ukiwa kitandani umelala peke yako. Lakini ukishakuwa na mwenzako huwezi kufanya hivyo lazima umshirikishe. Na katika kumshirikisha kuna kukataliwa au kukubaliwa.

Wakati huu ndio unaweza kuingia kwenye biashara na kufanya mambo makubwa sana. Kama wewe nib inti huu ndio wakati wako wa kuonyesha kile kilichopo ndani yako. Ukishaolewa unakuwa na nafasi lakini ni ndogo. Wakati wa kupambana ni ujananani.
Fanya maamuzi, chukua hatua, timiza ndoto yako. Muda unakimbia sana Rafiki, muda haukusubiri, usisema utafanya jambo Fulani ukishaoa au kuolewa unaweza kufika huko na ukakutana na vikwazo vikubwa kuliko ulivyowahi kutarajia.
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Jacob Mushi,
Author, Entrepreneur, Trainer, Life Coach,
Simu: 0654 726 668,
Twitter: jacobmushitz
Instagram: jacobmushi
Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading