Jinsi ya Kukuza Biashara yako.

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read
Habari za Jumapili ndugu msomaji wetu. Leo tutakwenda kuona ni jinsi gani unavyoweza kutengeneza wateja kwenye mtandao wako wa blog au mitandao ya kijamii.  Kama kawaida tumeshasema kwenye hii mitandao imebeba watu wa kila aina watu wa rika zote ni wewe tu ujue unawezaje kuwafikishia huduma/bidhaa yako.

Hapa tutakwenda kuona njia mbalimbali:
1. Toa maelezo jinsi gani mteja wako anavyoweza kufaidika na bidhaa/huduma yako. Hapa utaenda kuelezea kwa maneno rahisi ambayo kila mtu akisoma ataelewa bila tatizo. Kama tunavyojua wewe mtoa huduma ndie unafahamu vyema kuliko mtu mwingine.

2. Hakikisha uonekane unasaidia watu sio watu wakupa msaada kwa kuja kwako. Yaani kama ni huduma elezsa jinsi mteja anavyoweza kufaidika nayo na kama ni bidhaa vile vile.
3. Uaminifu. Uaminifu ndio kila kitu kwenye hii biashara ya kwenye mtandao maana mtu ananunua bidhaa kwako na hamjuani wala hamjawahi kuonana. Ukishindwa kua mwaminifu hii biashara haikufai na utakua unajiharibia mwenyewe. Mteja amelipia huduma/bidhaa hakikisha anaipata kwa wakati na inayolingana na thamani ya pesa yake. Hapa ukiweza utajijengea biashara kubwa sana. Watu wengi wanashindwa kwenye Uaminifu.

4. Jifunze kila siku juu ya biashara yako. Ukijifunza kila siku itakusaidia wewe kufahamu mambo mengi zaidi juu ya biashara yako na hii italeta ukuaji wa biashara.
 Kama tulivyosema tangu mwanzo kwamba hii ni biashara unaanza kuijenga utapata wateja wachache utahisi unapoteza muda lakini ukivumilia utayaona matunda utafikia kipindi wewe mwenyewe utajipongeza kwa uvumilivu wako. Mafanikio ya kweli na ya kudumu hayataki haraka lazima upitie changamoto mbalimbali lazima upoteze baadhi ya vitu ili upate vitu vizuri zaidi.
Asante sana nikutakie weekend njema.
©Jacob Mushi 2016
Tuandikie jacob@jacobmushi.com

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading