JINSI YA KUMALIZA MWAKA KWA USHINDI.

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read
Habari za Leo mwanamafanikio?  Siku kuu imekwenda vyema kwangu. Natumaini na kwako pia. Ni siku chache zimebaki katika mwaka  lakini tukiweza kuzitumia vyema tutaacha alama ndani ya mwaka huu.
 
Usikubali kabisa kutumia muda huu hovyo Tafuta jambo dogo tu la tofauti ulifanye
Zikiwa zimebaki takribani siku nne peke yake tumalize mwaka huu napenda kukwambia bado unayo nafasi ya kufanya kitu ndani ya mwaka huu.
Bado unayo nafasi ya kuacha alama mwaka huu. Unamaliza vipi mwaka huu?  Ni kitu gani hasa ufanye ili mwaka uishe kwa Ushindi? 
Inawezekana ulishakata tamaa kabisa ukasema ngoja tu tuanze mwaka  mpya nitaanza upya.  Usikate tamaa nafasi unayo.
Embu fanya kitu hata kama ni kidogo. Lakini kiache alama mwaka huu. Fanya maamuzi sasa uache nyayo mwaka huu.
Ni muhimu sana kufahamu kwamba siku moja unayoipoteza ina thamani kubwa sana. Usikubali kabisa kusema mwaka umeshaisha hivyo!  Basi tu malengo hayajatimia. Ntafanya tena mwakani.
Kiukweli mimi sijui wewe Unafanya kitu gani ningeweza kukwambia ufanye nini ili uache alama mwaka huu. Lakini mimi naweza kukwambia Fanya kitu hata kama ni kidogo.
Jaribu kuathiri maisha ya mwanadamu Mwingine kwa namna chanya. Gusa maisha ya mwingine kwa bidhaa yako unayoitoa. Gusa maisha ya wengine kwa huduma unayoitoa.
Jaribu kufikiria ni kitu gani hujawahi kukifanya kwa mteja Wako umfanyie kabla hatujamaliza mwaka. Jaribu kuangalia kila kona ni Sehemu gani unaweza kuitumia ili ufanye kitu cha tofauti katika kumaliza mwaka huu.
Karibu sana. 

Jacob Mushi
Entrepreneur & Author

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading