JIPONGEZE.

Unapotimiza malengo yako haijalishi ni madogo kiasi gani unatakiwa ujipongeze.
Kwanini ujipongeze?  Hii inakuongezea hamasa zaidi ya kufanya mambo mengine yanayoendelea.

Haijalishi ni Hatua gani umefikia jijengee tabia hii ya kujipongeza mwenyewe hakuna mtu mwingine atakuja akupe pongezi sana sana utaambiwa hongera.

Jipatie zawadi ndogo ndogo zile unazozipenda. Haina maana kwamba ukajipe zawadi kubwa ya gharama unaweza kujifanyia zawadi ndogo ndogo tu za kawaida.

Faida za kujipongeza:
1. Furaha
Hapa utajitengenezea furaha yako mwenyewe hivyo utajiona wa thamani mwenyewe hata usipopongezwa na wengine wewe bado utakua na furaha.

2. Hamasa ya kufanya zaidi.
Kama tunavyojua mwanadamu akifurahi hua anafanya zaidi. Hivyo unapojipongeza kwa zawadi hamasa yako itaongezeka na utaweza kutimiza malengo mengine uliyojiwekea.

3. Kusogea hatua nyingine.
Kadiri unavyoweza kufanikiwa kupiga hatua moja haijalishi ni ndogo kiasi gani jipongeze. Kuna wakati utaweza kusonga mbele hata mambo yakiwa magumu utakua na uwezo wa kufanya bila kuchoka.

Hakuna mtu mwingine atakuja kukupatia furaha hivyo furaha yako unaweza kujitengenezea mwenyewe kwa kujipa pingezi ndogo ndogo kwa kila hatua unayopiga.

Karibu sana
Jacob Mushi

This entry was posted in BIASHARA NA UJASIRIAMALI on by .

About jacobmushi

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *