Jiulize maswali haya kwenye chochote unachokifanya ili uongeze ubora.

jacobmushi
3 Min Read
Habari za leo rafiki yangu mpendwa ni furaha yangu kuona wewe ni mzima na umeweza kusoma ujumbe huu leo. 
Leo tunakwenda kuona juu vitu vya muhimu kujiuliza kwenye chochote kile unachokifanya iwe ni ajira, biashara binafsi, upo chuoni unasoma, kwenye ndoa yako, mahusiano yako na wengine. Ili uweze kua bora zaidi klna kuliko mtu yeyote lazima uweze kujiuliza maswali na uyapatie majibu na yale majibu uyafanyie kazi. Anza leo kujiuliza maswali haya: 


1. Kuna watu wengine wanafanya kile unachokifanya wewe?  
Jiulize swali hili na ulijibu kwa kuandika chini hata kama ni wafanyakazi wenzako au wafanyabiashara wenzako, wanandoa unaowafahamu.  Ukweli ni kwamba hakuna mtu ambaye anafanya kitu cha peke yake huku duniani chochote unachokifanya kuna wengine wanakifanya au walishakifanya.  Unapojiuliza swali hili litakupa mwangaza ujione kua hauko mwenyewe. 

2. Wanakifanya vizuri? 
Jiulize tena je kile ambacho wenzangu wanakifanya na mimi nakifanya pia je wanakifanya vizuri wanakifanya kwa ubora kama ni ndio andika pia kwenye pia kwenye kitabu chako. 

3. Wanakifanya vizuri kuliko ninavyokifanya mimi? 
Hapa ndio kuna majibu ya tofauti tofauti na kwa kua na umakini zaidi. Kama kuna wengine wanafanya kile unachokifanya je wanakifanyaje ni waimbaji wenzako wanaimba kwa ubora kuliko wewe? Wafanyakazi wenzako, wafanyabiashara na kila sehemu uliyoandika wewe. Hapa unafanya tathimini ya matokeo gani unayapata na matokeo gani wanayopata wao ndio utajua ni nani ni bora zaidi. Ukweli ni kwamba huwezi kuanza leo na kua bora leo kila kitu kuna hatua zake cha muhimu ni wewe kutambua kwamba unataka kuelekea kwenye ubora. 

4. Ninaweza kua bora kuliko wao?  
Kama ulipata jibu la kua wao ndio bora kuliko ni sasa ujiulize je unaweza kua bora kuliko wao,  jibu ni ndio unaweza na ni kwa kujifunza na kufanya. Kama wewe tayari ni bora kuliko wao.  Jifunze kuweza kubakia kwenye ubora na kusonga mbele zaidi. 

5. Matokeo yatakua ni nini kama nikiwa bora zaidi yao. 
Wewe ni mfanyakazi ukiwa bora zaidi ya wengine utapanda cheo,  mfanyabiashara biashara yako itakua kwa sababu wateja wakua wengi zaidi. Kila mmoja anaweza kujipa majibu kutokana na kile anachokifanya. 

6. Nisipokua bora matokeo yakua ni nini? 
Kama hutakua bora majibu ni kwamba utabakia hivyo hivyo ulivyo siku zote,  kama ni biashara inaweza kufa kwa sababu utapoteza wateja, kazini unaweza kupunguzwa endapo kumetokea kitu kama hicho. Ubora ndio kila kitu ubora ndio unaleta maendeleo ubora ndio unaleta uvumbuzi mpya kila siku. 

Hatufanyi kwa ubora ili kushindana, hatujiulizi maswali haya ili kushindana kiukweli kwenye zama hizi za teknolojia ukizubaa kidogo wewe na biashara yako hata kama ilikua kubwa kiasi gani mnapotezwa kwenye soko. Na hii ni pale mwenzako anapoweza kufikiri kwa ubora zaidi yako na akafanyia kazi mawazo yake. 

Asante sana na Karibu. 
Jacob Mushi 2016 
Niandikie 0654726668 Whatsapp, E-mail jacob@jacobmushi.com

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading