Kwenye Maisha tunakutana na watu wa aina mbalimbali ambao wengine wanaweza kuwa ni marafiki na wengine wanakuwa maadui. Mojawapo ya watu ambao utakutana nao ni watu wanaopenda kupokea bila ya kutoa chochote. Yaani mtu wa aina hii tunaweza kumwita kupe.
Mtu wa aina hii anapokutana na wewe ukamwona amehamasika sana anaongea maneno mengi sana ya kukupamba ili aweze kupata nafasi ya uaminifu kwako. Sio wote wanaoongea mameno mengi wako hivi ila unapaswa kuwa makini.
Watu wa aina hii wanapokuja kwako wanakuwa na lengo maalumu tu na wewe. Wakishamaliza uhitaji wao hutawaona tena. Unaweza kufikiri mligombana kumbe mwenzako alishapata alichokuwa anakitaka. Mtu wa aina hii inawezekana anataka kukukopa labda mnafahamiana lakini mmekuwa hamwasiliani muda mrefu.
Mtu wa aina hii anaangalia maslahi yake binafsi bila kuangalia wewe unafaidika nini kutoka kwake. Rafiki yangu ukikutana na mtu wa aina hii usikubali kuwa muwazi sana kwake. Usikubali kumwamini kirahisi. Akishaona huna manufaa yeyote na yeye atakuacha. Akiona amefanikiwa kupata alichokifata atakuacha bila ya taarifa.
Jinsi ya Kuwaepuka watu hawa.
Tengeneza tabia ya kuwa na mipaka kwenye Maisha yako.
Usiwe muwazi kwa kila mtu.
Kuwa na muda ambao unajua huu kwa uvumilivu wa mtu huyu naweza kumwamini.
Kuwa na vipimo ambavyo unaweza kumpa mtu anaekuja kwako akijifanya ni rafiki. Vipimo hivi vinaweza kuwa kama majaribio akiyashinda utajua umpe nafasi gani kwako.
Usikubali kumwamini mtu kirahisi kwasababu ya maneno yake mazuri.
Kamwe usikubali kuwa na tabia kama za mtu huyu moja kwa moja utakuwa unawavuta watu wa aina hii kwenye Maisha yako.
Kabla hujatamani kupata chochote kwa mtu jiulize wewe una kitu gani ambacho unaweza kukitoa ili usiwe mnyonyaji?
Usikubali kupokea pokea vitu vya bure mara nyingi inaweza kuwa ni mitego. Kama huwezi kukilipia ni bora usipokee hasa kwa watu usiowafahamu.
Unaweza usinielewe hapa, usipende kupokea offa hasa kama unajua hiyo offa huwezi kuja kuilipia endapo litatokea tatizo lolote.
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Jacob Mushi,
Author, Entrepreneur, Trainer, Life Coach,
Simu: 0654 726 668,
Twitter: jacobmushitz
Instagram: jacobmushi
Facebook: Jacob Mushi Page
Barua pepe: jacob@jacobmushi.com