479; Kabla Hujakata Tamaa, Jaribu Njia Nyingine.

jacobmushi
2 Min Read

Kuna Wakati wale uliowatarajia Wakusaidie watakugeuzia Mgongo. Usiogope, Usilaumu, Usilalamike Mtumaini Mungu, na Jaribu Njia Nyingine.

Mwaka 2016 nilijitoa muhanga wa kutafuta mtaji wa kufanyia biashara. Niliingia kwenye simu yangu nikaona nina namba zisizopungua elfu moja.

Katika hizo namba watu Karibu 500 walikuwa wananifahamu. Nikasema ngoja niwatumie watu hawa kukusanya mtaji.

Nikaandaa ujumbe mzuri nikawatumia niliwaomba wanichangie tsh elfu mbili tu (2000/=) ili niweze kukusanya tsh milioni moja jumla kwa watu mia tano.

Hawa watu hawakuwa matajiri ni watu wa kawaida tu niliokuwa nawafahamu. Hivyo niliona kabisa hakuna atakaeshindwa kunichangia tsh elfu mbili.

Kiukweli nilianza kutuma ujumbe baadhi ya watu walifurahi, Wengine hawakujibu sms kabisa. Wapo ambao walinichangia na nikafanikiwa kukusanya tsh laki mbili.

Pesa ile nikaiwekeza kwenye vitabu kwasababu haikutosha kwenye lile wazo langu la biashara.

Kwanini nimekueleza hili?
Kuna watu hawatakaa wapende mafanikio yako.
Kuna watu hawatakaa wanunue unachouza.
Kuna watu hawataki kabisa Kukuchangia kwenye kitu cha maana lakini wapo tayari kuja kusherehekea mafanikio yako.

Wale walionichangia asilimia kubwa sikuwa nawafahamu ilitokea tu Rafiki Yangu alienielewa sana alinielezea kwenye kundi lake na watu wakajitokeza kunichangia.

Lolote unalolipanga halitakuwa kama ulivyotarajia.
Nilidhani elfu mbili ni ndogo basi wote watatuma haraka na kunipongeza lakini ikawa tofauti hata niliotarajia watachanga walikataa hata kupokea simu zangu.

Sijakata tamaa na wala siwezi kukata tamaa mpaka mwisho.

Wewe umeshaamua kujaribu njia gani?
Kabla Hujasema umekata tamaa jiulize umejaribu njia ngapi.

Naomba utambue pia wale unaotarajia wakusaidie ndio wanaweza kugeuka wakati unahitaji msaada wao.
Jipange kwa hayo, jiandae kuumizwa.

Kuwa imara ili Usiishie Njiani.

Nakutakia Kila la Kheri katika Uthubutu.
@jacobmushi
www.jacobmushi.com

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
1 Comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading