Habari za leo ndugu msomaji wa makala hizi. Jana nimepokea ujumbe kutoka kwa rafiki yetu ambaye hua anasoma makala hizi kila siku. Akaniomba niandike kuhusu vijana. Kijana tunaweza kusema ni mtu mwenye umri kuannzia miaka 18 hadi 40. Hivyo kama upo hapo lazima uzitumie vyema fursa hizi.

Leo tutaangalia Fursa tulizonazo sisi kama vijana na tunavyoweza kuzitumia kufanikiwa kwenye maisha yetu.

MUDA.
Muda ni fursa ya kipekee ambayo tumepewa hapa duniani kwa usawa wote tuna masaa 24. Ukiachana masaa 24 ni kwamba kuna kingine cha kipekee kwako wewe Kijana unatofautiana sana na mzee mwenye miaka 50 mzee huyu muda umeenda hana muda wa kutosha kuamua kuhusu maisha yake japo pia siyo sababu hiyo. Kama una miaka 20 sasa ni kwamba una miaka mingine 10-20  ya kua tajiri.
Unautumiaje muda huu wa ujana wako kuweza kubadili maisha yako?  Ni wakati wa kukaa chini ujue umebakiza muda gani ili uuache ujana uhamie kwenye uzee na utautumiaje muda huo kufanya kitu cha tofauti ili uache alama kwenye ujana wako. Kaa chini fikiria sawasawa na utaona ni nini cha kufanya. Kuna watu nusu ya ujana wao wametumia kuangali movies, mpira, kusoma magazeti ya udaku, kufanya uzinzi n.k. badilisha mtazamo wako leo acha kulalamika mtaji huna Muda ni mtaji wa kwanza.

NGUVU.
Fursa nyingine ya kipekee tuliyonayo ni Nguvu.  Sisi vijana tuna nguvu na miili yetu ina afya bora.
Kuna kazi ambazo wewe unaweza kuzifanya lakini mtu mwenye miaka 50 hawezi maana hana nguvu.
Kuna sehemu unaweza kutembea kwa miguu na ukafika bila kuchoka lakini mzee hawezi.
Nguvu ni mtaji wa pekee sana tukitumia nguvu zetu vyema zitatuletea mafanikio.
Kitabu cha mithali kinasema “Usiwape wanawake nguvu zako”
Kwamba nguvu ulizonazo unaweza kuzitumia na kuzimalizia kwenye matendo maovu au ukazitumia kubadili maisha yako ni wakati wako wa kuamua tu.
Kuna watu wanatumia nguvu zao kupigana, kuiba, na kufanya vitu visivyo leta matokeo bora kwenye maisha yao.
Anza leo kutumia mtaji huuvwa nguvu ubadili maisha yako.

UWEZO WA KUFIKIRI.
Kama kijana uwezo wako wa kufikiri na kufanya maamuzi ni mkubwa kuliko wa  mzee sina maana ya kusema wazee hawana uwezo wa kufikiri la hasha! Ninachosema ni kwamba mzee akili yake imepitia mengi, imeamua mengi, imekosea pia sana. Lakini kwa kijana ana nafasi kubwa ya kujifunza na kuweza kufikiri sawasawa na kufanya maamuzi sahihi. Akili ya kijana bado ni fresh ni mpya kwa hiyo ikitumika vyema italeta matokeo makubwa kwenye maisha yetu.
Akili ya kijana ina uwezo wa kuvumbua Mawazo mapya. Tukiangalia wavumbuzi wa vitu mbali mbali wengi wa kipindi hikinni vijana.
Tutumie uwezo huu kufikiri vyema kubuni na kuchukua hatua tubadili maisha yetu.

MUDA, NGUVU, NA  UWEZO WA KUFIKIRI ukichanganya kwa pamoja kijana unaweza kufanya mambo makubwa. Unaweza kubadili hali yeyote kwenye maisha yako. Jifunze sana kwa kipindi hiki na yale unayopitia.
Acha kulalamika na kulaumu. Chukua majukumu yote ya maisha. Anza kua kiongozi wa maisha yako mwenyewe.
Maisha yako yatabadilika.

Asante sana
Mushi Jacob

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading