KONA YA BIASHARA: Lijue Dhumuni La Biashara Yako.

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read

Kama jinsi kulivyo na magari ya abiria, mizigo na binasfi vile vile biashara zipo kwa madhumuni ya aina mbalimbali. Ni vyema wewe kama mfanyabiashara ukalijua dhumuni la biashara yako kwenye jamii uliyopo.

Jiulize unawasaidia nini watu kwa biashara yako?

Unajua mtu hawezi kwenda kununua gari la abiria wakati mahitaji yake ni gari la kutembelea. Hivyo wewe ukiweza kujua dhumuni la biashara yako utaweza kujua yafuatayo:

Utawafahamu wateja wako ni wakina nani.

Utajua namna ya kuwahudumia vzuri kama ukiwafahamu.

Kama wewe unauza maji ya kunywa dhumuni la biashara yako linaweza kuwa ni kuwasadia watu watoe kiu cha maji. Lakini unapaswa kuenda mbele Zaidi, kwasababu hao watu wangeweza kuchota maji ya bombani. Sasa kama upo sehemu ambayo maji yanapatikana kwa shida tunasema unawarahisishia watu kupata huduma ya maji.

Dhumuni la biashara yako kwenye jamii ni lile tatizo inalokwenda kutatua au kupunguza kwenye jamii. Ni ile namna unavyokwenda kumsaidia mteja wako.

Ukilijua dhumuni la biashara yako unaanza kupata mwangaza mzuri wa kuikuza biashara na kuwafikia watu wengi Zaidi.

Ukitoka nje ya dhumuni unajikuta unaongeza matatizo badala ya kutatua matatizo. Watu wanakuja kwenye biashara yako halafu wanaondoka na hasira, hapo umeongeza matatizo.

Ukiliacha dhumuni la biashara yako unakuwa wa kawaida kama wengine nah apo ndio mwanzo wa kuanguka kibiashara.

Lijue Dhumuni na Lifanyie Kazi kwa Viwango vya Juu.

Jacob Mushi,

Author, Entrepreneur, Trainer, Life Coach,

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading