Kinachofanya ubaki kwenye soko sio jina lako kubwa ulilonalo, sio bidhaa yako nzuri peke yake. Kuna vitu vya ziada lazima ufanye ili uendelee kubaki. Bahati mbaya sana usipofanya yupo mwenzako ana biashara kama yako atafanya na atakuchukulia wateja wako.

Bahati mbaya sana kama unafikiri huna mshindani bado hata kesho unaweza kumuona mtu mwingine amekuja hapo ulipo na akaanzisha biashara kama yako na akafanya vizuri kuliko wewe kisha akachukua wateja wako.

Usijitie kiburi eti kwasababu upo wewe hakuna mahali kwingine mteja atakwenda. Hivyo badala ya kufanya huduma nzuri basi unafanya hovyo hovyo. Watu wameweka vidonda moyoni mwao. Wateja wanavumilia dharau zako ipo siku watakuonyesha na wao wananguvu Zaidi yako.

Wewe kama mfanya biashara neon samahani linatakiwa liwe karibu ya mdomo wako kuliko hata unavyokumbuka kurudisha chenji. Kwanza neon hili halikugharimu kitu chochote. Unapogundua umemfanyia mteja ndivyo sivyo hadi akafikia kulalamika usisite kusema samahani.

Hata kama mteja wako amekosea yeye usibishane nae penda sana kutumia busara kumaliza tatizo na usipende kuonekana wewe huna makossa mbele ya mteja wako. Unajua kwanini? Wako watu wanakutazama watachukulia kwa picha mbaya wakikuona una majibu ya kejeli kwa wateja wako.

Mfano unamwambia mteja “ondoka hata pesa yako sitaki,” “nenda kwenye maduka mengine” ukija hapa sitakuhudumia” ndio unaweza kufikiri umemkomoa lakini kwa kauli zako tu hizo zinaweza kuwafanya watu waogope kuja hapo dukani kwako. Wateja wengine watasema kumbe na mimi nikikosea atanijibu hivi.

Badala ya kujibizana na mteja wako wewe shuka chini msikilize ikiwezekana mfanyie kitu kizuri ambacho ataona aibu mwenyewe. Ni kweli wapo wateja wasumbufu sana lakini ni bora ukatumia busara kumalizana nae kuliko maneno mabaya kama ya kumfukuza.

NENO SAMAHANI LISIWE MBALI SANA NA MDOMO WAKO.

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading