Ili uweze kua na ndoto,  maono,  malengo,  mipango,  au chochote kile Unachokitaka kwenye maisha yako.  Ni lazima kwanza uanze kujua unataka nini.
: Bila kujua unataka nini  utajikuta kila kinachokuja unafanya.
Tuna wanafunzi walio maliza form six na wengine watakwenda kumaliza form four
: Mara nyingi nimekua naona wengi wanafanya maamuzi tu kwa kile kilicho kirahisi.  Mfano  umepata grade  ambazo sio rafiki sana unaishia kuchagua kozi ambayo itakupatia  kazi kirahisi
Tangu ukiwa mdogo ndoto yako ilikua ni uje kua rubani leo hii kwakua umepata grade  chache unaamua kua mwalimu

: Au kwa kua umefeli form ukaenda kua askari kwa vile ajira zipo nje nje
 Utakuja kutupiga mabomu bure sisi kumbe haikua mpango wako wa kua askari ?????
 Inawezekana labda umekua hapo ulipo kwa msukumo wa wazazi wako na sio kutoka ndani yako. Unafanyaje kutoka hapo ulipo.?
Umekua mwanajeshi kwa vile kwenu kuna mtu mkubwa jeshini atakusaidia kupata cheo kizuri.?
: Huwezi kubadili hyo kwa sasa unachotakiwa kujua uchukue hatua gani sasa ili ufikie kile ulichokua unakitaka

: Kama ulikua upo kwenye mtego huo wazazi wanakulazimisha ukasomee kozi fulani ina kazi haraka hutateseka kupata kazi ni wakati wako kujitambua na ukaanza kubadili uendee kule unakokutaka.
Tuachane na hayo sasa naomba nitoe dakika moja kila mmoja atafakari anataka nini?  Unataka kuja kua nani?  Najua inawezekana umeshakua je hapi ndio mwisho?  Unahitaji kupiga hatua zaidi ya hapo!  Dunia inapaswa ikujue!
Ni naio humu ndani yeye hatamani kua mtu mkuu yeye anatamani awe mtu wa kawaida tu anyooshe kidole tumwone

“If your priorities don’t get scheduled into your
               planner, other people’s priorities will get put into your planner.”
                Robin Sharma

Unataka  kua Rais wa nchi.  Unafanya nini kila siku ili ufikie  hiyo ndoto yako. Kama wewe muda mwingi unautumia kufuatilia mpira zaidi kuliko siasa utakua Raisi wa namna gani?

 Kama wewe unataka  kua mwimbaji bora halafu muda mwingi upo kwenye mpira unafikiri utakua mwimbaji wa namna gani?

Kama wewe husomi vitabu vinavyohusu kile Unachokitaka  hujifunzi hata kidogo unafikiri utafikiaje kule unakokutaka?  Utaendaje bila ujuzi?
Muda wako mwingi  unautumia kufanya nini?

If you change your thinking, then you will change your actions, and if you change
your actions, then you are going to change your results.

 “We first make out habits, and then our habits make us.” (John Dryden)

 Tunatengeneza tabia ambazo hazitufikishi kule tunakotaka kwenda.

 “Any act often repeated soon forms a habit; and habit allowed, steadily gains in
strength. At first it may be as a spider’s web, easily broken through, but if not
resisted, it soon binds us with chains of steel.” (Tryon Edwards)

Tabia ni vile vitu vidogo vidogo tunavyofanya kila siku.  Unaporudia jambo kila mara linajengeka na kua tabia na linayegeneza mfumo wa maisha yako na mfumo unakuletea hatma

Ukitaka kubadili hatma anza kubadili  vitu unavyoingiza kwenye akili yako.  Lisha akili yako vitu ambavyo unataka vikuletee matoke uyapendayo.

Sijasema usifuatilia vitu vingine lakini kua na mipaka lazima ujue kuchagua.  Lazima ujue hiki kinahitajika kwa wingi kiasi gani.
Kama vile mwili wako unavyohitaji mlo kamili hvyo hivyo na akili pia  Wewe siku nzima unafuatilia siasa halafu nikikuuliza  unataka  kuja kua nani kwenye  siasa.  Huna hata mpango wa kua mwenyekiti wa kijiji?

 Unafahamu wachezaji wengi wa ulaya nikikuuliza  unampango na malengo gani kwenye  mpira  hujawahi kufikiria hata kucheza ligi ya mtaani kwenu

Unafahamu  nyimbo zote alizotoa mwanamuziki  na kuziimba nikikuuliza una malengo na mpango gani kwenye mziki hujui wala huna mpango wowote

Badili tabia zako ili ufikie mafanikio,

Karibu sana,
Jacob Mushi
0654726668

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading