Leo Ndio Yako…

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read

Habari ndugu msomaji wa makala zetu. Ni matumaini yangu unaendelea vyema na mapambano ya maisha. Tunamshukuru Mungu tunapokea ujumbe kwenu kua makala hizi zinafundisha. Tutaendelea kufanya hivyo kwa utukufu wa Mungu.

Leo ndio yako  huna siku nyingine uliyonamatumaini nayo zaidi ya leo. Kwa kama kuna jambo umeliweka kwenye ratiba ya leo lifanye kwa bidii zote maana haitarudi tena.

Leo ndio yako haina maana usiwe na mipango ya kesho. Kua na mipango na malengo ya maisha yako yote lakini jua kua unaishi leo tu. Leo ndio uitumie kufanya na kutimiza malengo yako. Kama wanavyosema huwezi kumla tembo mzima kwa wakati mmoja lazima uanze na sehemu ndogo ndogo mwisho unakuta tembo mzima ameisha.

Leo ndio yako maisha hayahitaji papara nenda kwa mipango uliyoiweka sikiliza ushauri wa watu mbalimbali uchambue chukua vinavyofaa tambua kua unaishi leo tu. Hakuna siku utaamka ukute yale uliyokua unayatamani yametokea. Anza leo kufanya kidogo kidogo mwisho tembo mzima ataisha.

Kama ulikua hujaweka malengo na ndoto zako Leo Ndio Yako andija leo vitu vyote unavyopenda  kua navyo maishani. Unapenda kua nani n.k. kisha angalia ni vingapi unavyoweza kuanza kuvifanya leo. Anza navyo hvyo kidogo kidogo unakuta umemaliza tembo mzima usisubiri siku fulani ifike ndio uanze anza leo. Kama huna ajira fanya kazi yeyote cha msingi iwe na mchango katika kutimiza ndoto zako. Kama haina mchango ni sawa unapoteza muda.

Nina amini kua mimi siwezi kukwambia nini cha kufanya kwa kua unajua hivyo basi ni jukumu lako kuchukua hatua na kuomba ushauri pale unapokwama.

Asante sana kwa kusoma ujumbe huu. Ubarikiwe sana. Nitafurahi ukiniambia umejifunza kitu.
Imeandikwa na Jacob Mushi 0654726668 mushijcob@gmail.com

Kwa maoni na ushauri tuandikie riseshine500@gmail.com pia tembelea ukurasa wetu wa facebook Rise and Shine Tz.

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading