Habari za leo ndugu msomaji wetu leo tunaendelea na makala zetu karibu sana na samahani kwa kutokuwekwa kwa makala kwa siku kadhaa.
Maisha ni mafupi sana usichezee na muda hata kidogo tumia. Hakikisha una furaha kila siku usisubiri upate pesa ndo ufurahi furahia safari uliyonayo sasa.
Usikubali siku ipite bila kujifunza kitu kipya kwa maisha yako. Soma vitabu mbali mbali vya kujenga ufahamu. Sikiliza audios nzuri. Tazama video nzuri za kujifunza, Kwani muda ni mchache sana.
Kuwa mkweli hakikisha kila unachowaahidi watu unakitekeleza kwa kila unapoahidi mtu kitu na kutotekeleza unajijengea tabia ambayo itakua inakusumbua pia watu watakosa imani na wewe.
Kila dakika unayoipoteza kufikiria matatizo uliyonayo unapoteza nafasi ya kufikiria utatuzi wa matatizo yako. Badala ya kufikiria matatizo uliyonayo fikiria utatuzi wake. Kama ulikosea umeshakosea usiwaze wala kuogopa kuhusu makosa uliyoyafanya bali jifunze chukua lile ulilojifunza kutokana na makosa hayo. Huwezi kufuta makosa uliyoyafanya jana bali unaweza kufanya vizuri leo.
Bora kujaribu jambo na ukashindwa kuliko kutokujaribu kabisa kwani aliejaribu akashindwa ana uwezo mkubwa kuliko Yule ambaye hajajaribu chochote. Kila wazo zuri la maendeleo linakujia lifanye kama una uwezo wakulifanya. Utaongeza uwezo wako juu ya mambo mengi.
Jifunze kusema hapana kwenye mambo ambayo hujayawekea vipaumbele kwenye maisha yako hata kama hayo mambo ni mazuri kiasi gani. Hata kama aliekwambia ni mtu wako wa karibu sana. Usifanye kumridhisha huku wewe vipaumbele vyako ukaviacha. Jibidiishe kwenye mambo yanayokuletea faida kwenye malengo na ndoto zako. Wakati mwingine tunnakubaliana na mambo tu kwa sababu waliotuambia ni watu wa karibu na sisi lakini tunasahau na kuacha mambo ya muhimu katika kutimiza makusudi yetu ya hapa duniani.
             “If your priorities don’t get scheduled into your
               planner, other people’s priorities will get put into your planner.”
                Robin Sharma
Kuwa na muda wa kukaa peke yako na utafakari japo lisaa limoja kwa wiki kama upo bize sana ujitakari na uone unakoelekea. Unapokuwa na muda wako peke yako kuna mambo mengi utagundua kwenye maisha yako kuna vitu utaviona vya mbele. Kuna picha utakuwa unaipata kila siku juu ya maisha yako unapotafakari juu ya kusudi lako hapa duniani utaweza pia kugundua kama unakoelekea ndipo au sipo.
Jacob Mushi.
#UpoHaiKwasababuMaalumu.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading