Mambo ya muhimu yanayokurudisha nyuma kwenye kutimiza ndoto zako;
1. Watu unaoambatana nao.(Marafiki)
Watu unaoambatana nao ni sababu kubwa ya wewe kukurudisha nyuma
Huwezi kuambatana na marafiki waovu ambao hawazungumzi mambo ya maendeleo ukategemea kuaendelea mbele.
Mithali 18:24- Ajifanyiae rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe, lakini yupo rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.
Ili ufanikiwe unahitaji watu wanakusogeza mbele wanaokupa mawazo ya maendeleo na sio mawazo ya upotovu.
Soma 2Samweli 13 :5 kwenye mlango huu wa 13 tunaona nguvu ya ushawishi wa marafiki Yonadabu alimshawishi rafiki yake Amnoni ajifanye anaumwa ili aweze kuapata nafasi ya kufanya uzinzi na dad yake Tamari. Amnoni alimsikiliza rafiki yake na akaufanya upumbavu ule. Swali langu kwako ni marafiki gani ulio nao? Ni mambo gani hasa wanapenda kukushauri? Ukikaa nao ni mambo yapi wanapenda kuzungumza? Kazi ni yako kuchagua marafiki wanaofaa.
Mtu mmoja kasema “ukiambatana na wajinga tisa kwa hakika wewe utakuwa ni wa kumi”
2. Hofu.
Kwa kupitia tabia hii ya hofu unaweza kukosa vitu vingi sana katika maisha yako.
Hofu inakusababisha usijaribu kitu chochote
Kila unaloliwaza la maana unaogopa kufanya kisa kushindwa.
Jinsi ya kuondokana na tabia hii ni kuhakikisha kila mara unazungukwa na mawazo ya imani, na sio ya woga,ukiweza kufanya hivyo utakuwa na mawazo ya imani na matokeo ya kushinda na sio ya hofu na woga. Hofu ya kushindwa na hofu ya kukataliwa visikufanye uogope kufanya mambo unayoyataka. Waliokataliwa ndio walioleta mabadiliko na mapinduzi duniani Usiogope.
3. Kuridhika na hali uliyonayo.
Katika jambo jingine baya kuliko yote ni kuridhika na hali uliyonayo. Kuridhika na maisha unayoyaishi. Ukweli ni kwamba ukiridhika na hali uliyonayo huwezi kufanya jitihada za kusogea mbele. Kama umeajiriwa unalipwa mshahara mzuri unaweza kutimiza mahitaji yako yote. Ukiridika na hivyo hutakaa uweze kufanya mabo mengine tena. Dunia inabadilika kila siku mifumo inabadilika kama utazoea mfumo huo huo kuna siku utajikuta hauwezi tena kuingiza kipato. Una biashara inakuingizia kipato cha kutosha mahitaji yako yote ukiridhika nayo kuna siku llolote linaweza kutokea maishani. Unaweza ukakwama. Mabadiliko ya tecknolojia yanaweza kukukwamisha n.k. usiridhike na hali uliyonayo mambo yanabadilika na wewe nenda nayo ukizubaa utaachwa hapo.
Yapo mengi mno nimeona nikueleze hayo matatu tu kwa leo kesho tutaendelea na yaliyobaki
Jacob Mushi
#UpoHaiKwasababuMaalumu.