Mara nyingi tunakua tunatamani watu fulani wabadilike wawe katika hali fulani tunazozitaka sisi. Ukweli ni kwamba huwezi kumbadili mtu ila mtu anaamua kubadilika mwenyewe.
Mtu wa kwanza kuamua kubadilika yeye mwenyewe anatakiwa uwe ni wewe kabla hujatamani kuibadili dunia, kubadili pale unapoishi, kubadili marafiki ulionao anza kubadilika wewe.
Ukishabadilika kuba baadhi ya vitu vitakuacha vyenyewe, kuna baadhi ya watu wataona mabadiliko yako na wataanza kukaa mbali na vilevile utaanza kuwavutia wale unaofanana nao. Wengine wataanza kutamani kua kama wewe.
Huwezi kuibadili dunia ila unaweza kujibadisha wewe, utoke kwenye hali uliyonayo sasa hivi na usonge mbele zaidi.
Katika hatua za kuketa mabadiliko kwako wewe mwenyewe nako pia kuna changamoto zake maana unakwenda kuziacha tabia ambazo ulikua nazo muda mrefu sana na unakwenda kujenga tabia mpya. Kuna nguvu kubwa ya upinzani kati yako wewe na tabia zako za zamani. Sio kitu cha siku moja.
Kitu cha kufanya ziandike kwenye kitabu chako kidogo zile tabia ambazo Ungependa kuzibadili maishani mwako.
Anza na tabia mojamoja au angalau tabia mbili.
Andika madhara ya wewe kuendelea kua na tabia mbaya au hali ya maisha uliyonayo sasa
Andika ni vitu gani vipya utavipata ukiziacha tabia hizo.
Anza sasa kufanya vitendo kama ulikua unalala sana anza zoezi la kuamka mapema kila siku asubuhi saa kumi na moja alfajiri. Fanya hivi mfululizo ndani ya siku 21. Ukishindwa njiani anza tena hadi uweze kuamka siku 21 mfululizo.
Ukifanya hivi kwa muda mfululizo itakua ni tabia yako. Fanya hivyo kwa tabia yeyote unayotaka kubadili maisha mwako
Asante sana na Karibu
Jacob Mushi 2016
Niandikie 0654726668 Whatsapp na Email jacob@jacobmushi.com